MADOLE
PATA HABARI NA BURUDIKA
Tuesday, February 12, 2013
Friday, January 25, 2013
PICHA MBALIMBALI ZA MAANDAMANO YA WANACHUO WA ST.JOHN YALIYOFANYWA KATIKA SIKU YA JANA
| ||
Wanafunzi baada ya kusubili kwa muda mrefu kibari icho wakaamua kuandaa mabango kwa ajili ya maandamano, ambapo kibari kipatikane kisipatikane walidai kuandamana ni lazima |
Mabango yalipokamilika wakasimama kwenye bendera kwa mara nyingine |
Walifika mbali na kuona kuwa polisi wanahusika katika mambo mabaya wanayofanyiwa. Ndipo wakachora bango hili kuonyesha hisia zao |
Hapa wapo barabarani na masomo kwa siku ya leo hayakuwepo |
Bango lina picha ya mwanafunzi alieuliwa kikatili, aliefahamika kwa jina la LYDIA LEO |
Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia |
Haya huyu anaashiria demokrasia na maendelea ndio imetawala juu yao |
Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni |
Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala |
Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi |
Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo |
Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni |
Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho |
Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita |
Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration. |
Safari ya maandamano ya amani ikawa
imeishia chuoni hapo baada ya kuona kuwa ujumbe wao umefika. Wanafunzi
wa chuo wamechoshwa na matendo mabaya ambayo wanafanyiwa ikiwa ni pamoja
na kubakwa, kulawitiwa, kuibiwa vitu vyao kama Laptop na vitu vingine.
Wameonesha umoja wao kwa sababu ya kuchoshwa na mambo hayo, ambapo leo
asubuhi kuna wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop. Hivyo wakaamua
kujikusanya asubuhi hiyo hiyo mida ya saa kumi na mbili alfajili na
kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja ambaye walimpiga na baadae
kuchukuliwa na polisi.
Thursday, January 24, 2013
WANAFUNZI WA ST JOHN DODOMA ZAIDI YA 5000 WAMENDAMANA KATIKATI YA MJI WA DODOMA WAKIPINGA UBAKAJI NA ULAWITI:
Wanafunzi wa Saint John University wakiwa wamebeba mabango katika maandamano yaliyofanywa leo
Hivi ndivo ilivyokuwa katika mji wa Dodoma kufuatia maandamano wanafunzi wa Saint John University
Hayo ndiyo yalikuwa ya moyoni mwa wanafunzi wa chuo cha Saint John Dodoma




W anafunzi zaidi ya 5000 wa chuo cha Saint John Dodoma wameandamana leo kushinikiza Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma liwajibike katika matukio ya kiuhalifu yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yakiwemo mauaji yanayofanywa na vibaka na majambazi.
Maandamano hayo yamefanywa kutokana na kudaiwa na wanafunzi hao kuwa kumekuwa hakuna uwajibikaji wa Jeshi la Polisi katika usalama wao.
Jumatatu ya wiki hii nikimaanisha Tarehe 21 / January / 2013 mwanachuo aliuawa na kuporwa simu,siku ya jana katika Hosteli za akina dada zilivamiwa Laptop , simu na fedha ziliporwa, katika tukio hilo la jana wanfunzi walipigwa na kujeruhiwa vibaya.
Mkuu wa polisi mkoa wa Dodoma ameahidi kulifanyia kazi tatizo hilo na kuimarisha ulinzi chuoni hapo.
ULINZI WAIMALISHWA KWA WANAFUNZI WA IFM BAADA YA KASHFA YA UBAKAJI NA KUIBIWA NA VIBAKA
UONGOZI
wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamazi wa Fedha (IFMSO) cha
jijini Dar es Salaam, umesema hali ya usalama kwa sasa katika Hosteli za
Kigamboni inaridhisha.
Waziri
Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema jana kuwa tangu iundwe timu ya
polisi inayoshirikiana na wanafunzi hao hali imekuwa tulivu kwa kipindi
cha wiki moja iliyopita.
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena
katika hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya
ripoti ya timu hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya
Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
“Kuna amani sana, misako imefanyika lakini ripoti itatolewa Januari 30 na Kamanda Kova,” alisema Sarungi.
Kauli
ya Kiongozi huyo wa wanafunzi haikutofautina na ya Kamanda wa Polisi
mkoa wa Temeke, Englbert Kiondo, ambaye alisema taarifa inayohusu hali
ilivyo itatolewa na Kamanda Kova.
Kwa upande wa wakazi wa Kigamboni, walisema kuwa wameshuhudia polisi wakifanya doria maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kabla wanafunzi hawajaandamana.
Walisema
pia wameona polisi wakiwakamata wahalifu kwenye maeneo hayo kutokana na
misako wanayoifanya hali ambayo imeleta utulivu kwenye mji huo.
“Kwa
sasa kumetulia inawezekana wanasikilizia (wahalifu), likini ingetakiwa
polisi wawakamate wale vinara kwa sababu wanawafahamu” alisema Salum
Rashid mkazi wa eneo hilo.
Naye
mkazi mwingine anayejishughulisha na biashara ya kioski, alisema kuwa
kumekuwa na utulivu kwani hata wanafunzi ambao ndiyo wateja wake wakubwa
wanamwambia kuwa wanaweza kuacha vitu wakavikuta salama.
WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUCHOMA NYUMBA ZAO
Habari
iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa kundi kubwa la wananchi
waliojawa na ghazabu Wilayani Rufiji leo wamevamia kituo cha Polisi
Kibiti Wilayani humo na kuanzisha vurugu kubwa kufuatia raia mmoja
mkazi wa kijiji hicho kudaiwa kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni
kutokana na kipigo cha Polisi.
Chanzo
chetu cha Habari kutoka Kibiti kinatupasha kuwa,kijana huyo
aliyefariki kutokana na kipigo hicho afahamikae kwa jina la Hamis
Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam na taarifa hiyo
ilipowafikia wananchi hao ndipo wakachukua uamuzi wa kwenda kituoni
hapo na kuanzisha vurugu hizo.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa,hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za
Askari Polisi hao zilizopo jirani kabisa na kituo hicho, licha ya juhudi
za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya
Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni
umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Inaelezwa
kuwa hali imezidi kuwa tete katika eneo hilo huku Polisi wa Kibiti
wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu ya
machozi hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.
tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
NEW TRACK : NAY WA MITEGO - UTAVUNA ULICHOPANDA
SHINE RECORDS .....TUNA PENDA KUTANGULIZA SHUKRANI ZETU KWA WOTE AMBAO
MNATUJALI KWA MAMBO MENGI AMBAYO TUNAFANYA NA PIA TUNAPENDA KUOMBA
MSAMAHA KWA WOTE AMBAO TULIWAKERA NA KUTUHISI TUNAWADHARAU NA TUNAPENDA
KUTAMBULISHA NGOMA MPYA YA MSANII ..NEY WAMITEGO AMBAYO INA KWENDA NA
UJUMBE WA UTAVUNAULICHOPANDA........IKIWA IMEFANYIKA ....SHINE
RECORDS.....,,,,CHINI YA MR T....
Tuesday, January 22, 2013
SAKATA LA KAHABA ALIYEOKOKA......
Mwanamke
huyu alijitambua vyema na kukiri ndani ya nafsi yake kuwa hawezi
kuolewa na mwanaume yoyote yule maana jamii yote ilikuwa inamtambua
kwa uchangudoa wake......
Kwa
hiyo , ili kurahisisha mambo na kuifanya biashara yake iimarike,
mwanadada huyu aliamua kwenda hospitali kukitoa kizazi
chake.Hakutaka tena usumbufu wa kutoa mimba au kufikiria
kondomu......
Tangu wakati ule biashara yake iliimarika na wateja walizidi kumiminika.Baada ya miaka
kadhaa, Upako wa mwenyezi mungu ulimfikia kupitia kwa mtumishi
mmoja wa mungu ambaye alifanikiwa kumfanya aokoke na kuwa
mtumishi mzuri kanisani.....
Siku moja, mchungaji mmoja alimwita na kumwambia kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi mungu amenena na mimi na kunifunulia kuwa wewe ndo mke wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."
Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
"Kaka
yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa hujamsikia
vizuri.Naomba uniache tu maana sina mpango wowote wa kuolewa"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Mwanamke huyu aliendelea kuyapuuza maneno hayo na ndipo sakata hilo lilipomfikia Askofu wa kanisa hilo.....
Wakiwa mbele ya mchungaji,Mwanamke huyu alifunguka kwa uwazi mbele ya askofu na kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye alikuwa ni kahaba wa makahaba....
Askofu naye alifunguka na kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa kwa mambo yaliyopita.Mungu humsamehe mwanadamu kwa kuzifuta dhambi zake zote za nyuma na kumfanya awe mpya..!!!"
Mwanamke huyu alifunguka tena na kudai kuwa:
"Baba askofu, mimi nilishatoa kizazi changu wakati nikiwa kahaba, kwa hiyo sitaweza kuzaa tena"
Askofu aliishiwa pumzi baada ya kusikia hivyo.Hakuweza tena kusema kuhusu kusahau ya nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji na kumwamba:
"Vipi, bado kuna maono yoyote toka kwa mwenyezi mungu?"
Mchungaji alijibu ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."
Askofu ilibidi awaombee kwa sala maalumu.Hatimaye ndoa ikafungwa......Baada ya miezi michache tu, huyu mwanamke alibeba mimba.Yeye pamoja na mumewe waliongozana pamoja kwenda hospitalini, tena kwa yule yule doctor aliyekitoa kile kizazi......
Daktari alipomuona alifurahi akidhani kuwa pengine mteja wake kamletea mteja mwingine.....Doctor hakuamini masikio yake baada ya kuambiwa kuwa huyu mwanamke ni mjamzito na amekuja kujiandikisha clinic....
Hakika Mungu ni Muweza wa yote....
SOURCE;MPEKUZI
Subscribe to:
Posts (Atom)