Habari
iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa kundi kubwa la wananchi
waliojawa na ghazabu Wilayani Rufiji leo wamevamia kituo cha Polisi
Kibiti Wilayani humo na kuanzisha vurugu kubwa kufuatia raia mmoja
mkazi wa kijiji hicho kudaiwa kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni
kutokana na kipigo cha Polisi.
Chanzo
chetu cha Habari kutoka Kibiti kinatupasha kuwa,kijana huyo
aliyefariki kutokana na kipigo hicho afahamikae kwa jina la Hamis
Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam na taarifa hiyo
ilipowafikia wananchi hao ndipo wakachukua uamuzi wa kwenda kituoni
hapo na kuanzisha vurugu hizo.
Habari
zaidi zinaeleza kuwa,hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za
Askari Polisi hao zilizopo jirani kabisa na kituo hicho, licha ya juhudi
za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.
Aidha
wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya
Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni
umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.
Inaelezwa
kuwa hali imezidi kuwa tete katika eneo hilo huku Polisi wa Kibiti
wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu ya
machozi hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.
tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia.
No comments:
Post a Comment