Sunday, January 20, 2013

SAKATA LA GESI: MTWARA NI MABOMU NA RISASI ZA MOTO....



MABOMU na risasi za moto jana zilitawala katika mji wa Mtwara na vitongoji vyake baada ya wananchi kufanya maandamano makubwa kupinga ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam.
 
Maandamano hayo yaliandaliwa na Chama Cha Wananchi (CUF) na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho upande wa Bara, Julius Mtatiro, ambaye alifuatana na wabunge wa chama hicho wanaotoka mikoa ya kusini.

Maandamano hayo yamefanyika baada ya maandamano mengine makubwa yaliyofanyika Desemba 27 mwaka jana kwa lengo hilohilo, yakiwa yamendaliwa na vyama vinane vya siasa.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, maandamano ya jana yalifanyika huku wanawake wakiwa mstari wa mbele.
Chanzo cha kupigwa mabomu hayo kinaelezwa kuwa ni kukatika kwa umeme katika eneo ulikokuwa unafanyika mkutano wa hadhara wa CUF ambako wananchi waliahamaki na kuandamana kwenda ofisi za Tanesco Mtwara i kujua chanzo kukatika kwake.

Wakiwa njiani kuelekea Tanesco umati huo mkubwa wa wafuasi wa CUF ulikutana na Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) ambao waliamua kuwatawanya kwa mabomu na kupiga risasi za moto hewani.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mtatiro jana, lengo la kufanya maandamano na mkutano huo lilikuwa ni kupokea karatasi ya kupinga ujenzi wa bomba la gesi kwenda Dar es Salaam
Alisema akiwa katika mkutano huo alipokea saini 10,000 za wananchi wa mikoa ya kusini ambao wanapinga mpango huo wa serikali kuisafirisha gesi. 

Maandamano hayo yalihitimishwa na mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara na wabunge wa CUF waliokuwapo ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tabora, Magdalena Sakaya (Tabora), Mbunge wa Mkanyageni Habib Mnyaa, Salum Barwan (Lindi Mjini), Said Bungara "Bwege" Kilwa Kusini na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mtwara, Clara Mwituka.

Mtatiro alisema msingi wa hoja yao ni kujikita katika kuhakikisha gesi inatumika kwa faida ya taifa lakini kwa kutoa kipaumbele katika maeneo yaliyo nyuma katika maendeleo, kama kusini.


Watu wakamatwa mitaani

Kutokana na vurugu hizo inaelezwa kuwa zaidi ya watu 20 walitiwa mbaroni na jeshi la polisi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Mary Nzuki hakuweza kupatikana jana kwa simu yake ya kiganjani. 

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mtwara, Tutufye Mwakagamba alikiri kukamatwa kwa watu kadhaa katika vurugu hizo ingawa alimtaka mwandishi wa habari hizi amtafute baadaye.


“Ni kweli ndugu yangu kuna watu kadhaa tumewakamata katika vurugu zilizotokea leo (jana), lakini ninakuomba nitafute baadaye kwa sababu muda huu nipo katika mkutano wa CUF ambako kuna mvua kubwa inanyesha,” alisema Kamanda Mwakagamba.

Biashara zafungwa
Kutokana na maandamano hayo yaliyoambatana na vurugu biashara mbalimbali zilifungwa katika soko kuu la Mtwara na mitaani hali iliyowafanya wananchi kuwa katika wakati mgumu.

Magari ya CUF kila kona
Habari zinasema mkutano wa jana ulikuwa na shamrashara za aina yake na zaidi ya magari 14 yalisafirisha wafuasi wa CUF kutoka wilayani Tandahimba wakati magari mengine manane yalitokea wilayani Newala.

Wakati huohuo, Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (CCM), ameibuka na kuitaka serikali kutodharau madai ya wananchi wa mikoa ya kusini kuhusu suala la gesi.

Aliyasema hayo wiki chache baada ya wananchi wa Mkoa wa Mtwara kufanya maandamano ya amani kupinga ujenzi wa bomba la kusarisha gesi kutoka mkoani humo kwenda Dar es Salaam.

Dk. Ndugulile, alisema kwa mtazamo wake suala hilo lina sura mbili tofauti ambayo yote yana hoja za msingi ikiwamo umaskini wa mikoa ya kusini na tataizo la ajira kwa vijana

YANGA YAIBUTUA BLACK LEOPARD 3-2 ,TEGETE ATUPIA MBILI CHEKI PICHA:

5 


7 
Wachrezaji wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya kufunga goli la kwanza katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
1  
Mashabiki wa Yanga wakishangilia wakati timu yao ikicheza kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.
2 
Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Mchezaji wa timu ya Yanga Kabange Twite akimiliki mpira mbele ya Nkosiabo  Xakane mchezaji wa Black Leopards ya Afrika Kusini  .katika mchezo wa kirafiki uliokutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, timu ya Yanga imeshinda magoli 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini.
Goli la Yanga limefungwa na mchezaji Jerrison Tegete kwa penati katika kipindi cha kwanza baada ya Mchezaji Haruna Niyonzima kuangushwa katika eneo la hatari na mchezaji wa timu ya Black Leopards na kuongeza goli la tatu katika kipindi cha pili , Huku mchezaji Didier Kavumbagu akapachika goli la pili katika kipindi katika kipindi hichohicho cha pili cha mchezo.
Timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini imefanikiwa kupata magoli mawili katika kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa Yanga 3 na timu ya Black Leopards 2 mpaka mwisho wa mchezao huo.

Dr Slaa alipua bomu




















Adai serikali imeagiza mtambo wa kuhujumu mawasiliano ya wapinzani

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema kuwa amebaini kuwapo mpango wa serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya wapinzani kwa ajili ya kuhujumu uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Dk. Slaa ambaye ni mara yake ya pili kutoa tuhuma za CCM kuingiza mtambo wa kuingilia mawasiliano ya CHADEMA, alisema tayari ameshapata e-mail yenye kuonyesha thamani ya mtambo huo na kwamba utagharimu dola 850,000 za Marekani, karibu sawa na sh bil. 1.3.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua kongamano la vijana wa vyuo vikuu wa CHADEMA (Chaso), jijini Dar es Salaam, lililokuwa na lengo la kujitathmini na kupanga mikakati ya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2015 pamoja na kuwaapisha viongozi wapya wa shirikisho hilo.
Alisema tayari ameshaandika barua kwa mamlaka husika kuwajulisha hilo, lakini hadi sasa hawajajibu.
“Tuna ‘details’ na nyaraka nyingi zinazoonesha namna mtambo utakavyotumika kwa ajili ya kuwahujumu wapinzani na kwa kuwa tumeshaandika barua kwa mamlaka husika na hawajatujibu, kwa sasa sitaenda kwa undani zaidi juu ya hili. Subirini siku ifike nitaweka kila kitu hadharani,” alisema Dk. Slaa.
Alisema CCM kwa kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa, wamekuwa wakitengeneza propaganda mbalimbali za kutaka kumchafua yeye pamoja na CHADEMA, lengo likiwa kuwaondoa Watanzania katika ajenda za msingi za kupigania ukombozi.
Aliongeza kuwa, awali mahasimu wake kisiasa walikuja na propaganda kuwa amechukua mke wa mtu, kisha wakasema amedhulumu viwanja huko Mabwepande na sasa wameanzisha suala la kukopa sh milioni 140 ambalo alifafanua kwamba halina ukweli wowote.
“Wanawalisha maneno wale wanaokubali kununulika, msifikiri yale yanatoka midomoni mwao hapana, lakini watambue leo hakuna Mtanzania atakayehangaika na uongo unaotengenezwa kwa ajili ya kuwafanya wazidi kutawaliwa,” alisema Dk. Slaa.
Akizungumzia tuhuma za CCM na serikali kushirikiana kuingiza mtambo wa kuhujumu mawasiliano ya wapinzani, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alisema madai hayo ni ya uongo.
Akizungumzia vita dhidi ya ufisadi nchini Dk Slaa, alisema wanaojidanganya kwa kusema kwamba kwa sasa siyo agenda ya Watanzania, wamefilisika kimawazo kwa kuwa suala hilo halitanyamaziwa na CHADEMA mpaka wahusika watakapotiwa mbaroni.
“Kama wanataka tunyamaze kuhusu ufisadi basi waturudishie twiga waliowatorosha, fedha za EPA, mabilioni ya Uswisi na pia watuambie ni kina nani wanawaua tembo walio katika hifadhi zetu na kisha kusafirisha pembe kupitia bandari zinazolindwa na watu wanaolipwa kwa kodi za Watanzania… vinginevyo hakuna wa kutunyamazisha zaidi ya Mwenyezi Mungu,” alisema Dk. Slaa.
Akielezea sera ya majimbo na mafanikio ya mikutano ya chama hicho kwa mwaka 2012, Dk. Slaa, alisema imekuwa na mafanikio makubwa hasa baada ya wananchi kuzinduka na kuamua kudai haki za kutaka kunufaishwa na rasilimali zinazowazunguka.
Alisema miaka minane iliyopita wakati CHADEMA waliposema rasilimali za nchi zianze kunufaisha eneo husika kwanza, watu wengi hawakuelewa, lakini leo baada ya kufikiwa na ufahamu kupitia Operersheni za CHADEMA, maarufu kwa jina la M4C, kila eneo limezinduka na sasa serikali inaanza kuwaona watu hao kuwa maadui kwa kuwa wanadai kuthaminiwa.
“Nchi yetu kila eneo kuna rasilimali na hatusemi ziwanufaishe watu wa eneo husika tu, bali tunataka waanze wao na ziada ndiyo iende maeneo mengine, leo mnawaona Mtwara na Lindi wanapigania haki hiyo na maeneo mengine hivyo hivyo, kwa hiyo tuna haki ya kujivunia mafanikio ya kuwaelewesha wananchi juu ya kudai haki zao,” alisema Dk. Slaa.
Aliongeza kuwa, mwaka huu watahakikisha suala la mauaji holela ya raia wasio na hatia, halijirudii ikiwa ni pamoja na kuishinikiza serikali iunde tume huru ya kimahakama kufuatilia matukio yote ya mauaji yenye utata yanayohusishwa na harakati za kisiasa mwaka 2012.
Akizungumzia suala la kufukuzana ndani ya CHADEMA, Dk Slaa alisema hawataogopa kumfukuza mwanachama yeyote msaliti anayeenda kinyume na katiba ya chama hicho na kutolea mfano madiwani waliofukuzwa mkoani Arusha na wanachama wengine.
Alisema licha ya madiwani wa Arusha kujua walifukuzwa kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA, waliamua kwenda mahakamani kutaka kukisumbua chama, hali aliyosema mahakama haikuweza kukubaliana nao na sasa wanawajibika kulipa gharama za kesi na wakishindwa wataenda gerezani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CHADEMA, John Mnyika, aliitaka CCM imshauri Rais Jakaya Kikwete aunde tume huru kuchunguza mauaji mbalimbali ya kisiasa yanayotokea nchini badala ya kupanda jukwaani na kusema CHADEMA ndio wauaji.
Alisema kuwa kila siku Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba na viongozi wengine ndani ya chama chao wamekuwa wakitaka kuwaaminisha wananchi kuwa CHADEMA inahusika na mauaji ya kisiasa.
“Nape anasema CHADEMA wanahusika na mauaji ya kisiasa, Mwigulu naye hivyo hivyo, viongozi wengine ndani ya chama chao nao wanapiga kelele hizo hizo, sisi CHADEMA tunasema iundwe tume huru ya kimahakama wao wanaogopa, wanajua wataumbuka juu ya ufedhuli wao,” alisema Mnyika.
Aidha, alisema wamebaini CCM inachapisha kadi za CHADEMA na kisha kuwagawia wanachama wao ili kuwahadaa wananchi kuwa chama hichi kinakimbiwa.
“Unajua ukiona mtu anajidanganya mwenyewe, huyo inabidi umsikitikie kwa kuwa kila njia ya udanganyifu wao sasa imeshabainika katika mioyo ya Watanzania, na sasa wameona wajaribu kujiridhisha katika nafsi zao wakiwa katika mikutano ya hadhara kwa kupeana kadi walizochapisha wenyewe huku wakishangiliana,” alisema Mnyika.


source:tanzania daima