Thursday, January 10, 2013

Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
 JESHI LA POLISI TANZANIA





YAH: TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA
 VYOMBO VYA HABARI TAREHE 10/01/2013.
Watu kumi na tatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi  Mkoani Dodoma kwa tuhuma za mauaji yanayohusisha imani za kishirikina.
Watu hao wanashikiliwa kutokana na tukio la mauaji lililotokea siku ya Jumatano tarehe 09/01/2013 majira ya saa 04:00 mchana katika kitongoji cha Mtakuja kata ya  Chitemo katika Wilaya ya Mpwapwa.
Katika tukio hilo  walisababisha kifo cha mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la NELSON S/O NYAGULU mwenye umri wa miaka 32, mkulima wa Chitemo  kwa kupigwa na risasi ya Bunduki aina ya Gobore tumboni na mtu aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KALANI.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba tarehe 08/01/2013 huko katika kijiji cha Chitemo kulikuwa na mnada, ambapo mvua ilinyesha sehemu moja ya kitongoji cha Mtakuja, sehemu ambayo alikuwa  anaishi mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la LEONARD S/O NYAGALU, Miaka 70, Mgogo.
Kwa vile mvua hiyo haikunyesha sehemu kubwa katika kitongoji hicho inasemekana Mwenyekiti wa Kijiji JAVAN S/O MZAZI, Miaka 40, Mgogo, aliibua hoja kuwa kwa nini mvua inyeshe eneo moja tu analokaa Mzee huyo na kuacha kunyesha sehemu nyingine katika eneo hilo na kuwahamasisha wenzake kwenda kwa Mzee Nyagalu akawaeleze vizuri.
Majira ya 23.00 hrs usiku wakakusanyana na kuelekea kwa Mzee  Nyagalu, Walipofika Mzee huyo alisikia watu wakizungumza nyumbani kwake hivyo akavunja ukuta na akatoroka.
Inadaiwa kuwa kundi hilo lililokuwa limeongozana na Mwenyekiti wa Kijiji hicho waliingia ndani ya nyumba na kumkuta mke wa Mzee Leonard Nyagalu na kuanza kumpiga ili aonyeshe aliko mume wake, waliposhindwa kumpata wakabomoa nyumba na kuichoma moto.
Wakati wanafanya tukio hilo, walijitokeza watoto wa Mzee Leonard S/O Nyagalo, mmoja wao akiwa ni NELSON S/O NYAGALU, Miaka 32, Mgogo na ndipo nao wakaanza kupigwa.
Kwa mujibu wa watu walikuwa katika tukio hilo walisema ilisikika sauti ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la RASHID S/O KARANI akisema sasa mmetangaza vita na akafyatua gobore na risasi zikampata NELSON S/O NYAGALU tumboni zilizopelekea kupoteza maisha wakati anapata matibabu.
Baada ya kufyatua risasi toka katika gobole Bw. RASHID S/O KARANI aliwaaga wenzake kuwa anakwenda kujisalimisha Polisi lakini hadi sasa hajaonekana na jitihada za kumtafuta pamoja na silaha aliyotumia zinaendelea.
Majina ya wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kutokana na kushiriki katika tukio hilo  ni kama ifuatavyo:-
1.  Dickson S/O Chimosa, Miaka 52, Mgogo, Mkulima na Mkazi wa Chitemo.
2.  Javan S/O Mzazi, Miaka 44, Mgogo, Mwenyekiti wa Chitemo.
3.  Robert S/O Lusije, Miaka 51, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
4.  Donald S/O Mponi, Miaka 33, Mgogo, Mkulima na mkazi wa Chitemo.
5.  Daniel S/O Mwamba, Miaka 24, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
6.  Maneno S/O Ngaile, Miaka 36, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo
.
7.  Thomaso S/O Nyagalo, Miaka 28, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
8.  Gilbert S/O Lugaje, Miaka 39, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
9.  Aden S/O Simon, Miaka 33, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
10.      Malolo S/O Sanja, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
11.      Sospeter S/O Sanja, Miaka 35, Mgogo, Mkulima, Mkazi 
wa Chitemo.
12.      Jocktan S/O Chilomo, Miaka 40, Mgogo, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
13.      Keneth S/O Ngaile, Miaka 38, Mnyamwezi, Mkulima, Mkazi wa Chitemo.
Aidha siku ya Jumamosi tarehe 05/01/2013 majira ya 08:00 asubuhi kulikuwa na tukio la mauji  lililotokea katika Kitongoji cha Magungu, Kijiji cha Mpendo, Kata ya Mpendo Tarafa ya Kwa Mtoro Wilaya ya Chemba Mkoa wa Dodoma.
Ambapo mtoto mmoja aliyetambulika kwa jina la TONY S/O SOKOINE mwenye umri wa miaka miwili na nusu (2.5), mkazi wa Kijiji cha Mpendo alifariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa kuchomwa na kisu shingoni kilichorushwa na mtoto mwenzake aliyefahamika kwa jina la SOMEI S/O REMENDA mwenye umri wa miaka mine (4) mkazi wa Kijiji cha Mpendo.
Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha Kifo hicho ni kwamba marehemu na mtuhumiwa walikuwa wanacheza nje nyumbani kwao kwa akina SOKOINE S/O RENENDA ambapo mtuhumiwa alirusha kisu kwa lengo la kumuua ndege aliyekuwa juu ya mti  uliokuwa karibu na nyumba yao, ndipo kisu huchi kiligonga kwenye mti huo na wakati kinadondoka kilimjeruhi marehemu kwa kumchoma shingoni  na kusababisha kifo chake.
 
DAVID A. MISIME - ACP
                  KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA    

YOU’RE MORE IMPORTANT


YOURE MORE IMPORTANT
          Man is a social being; he interacts with many people from different areas.
           Looking around at where I am I see people, so many. Some I know some I know some I don’t; just different people. Looking at them closely I see one thing; they are all different; so are their thoughts, beliefs, goals and ideas. Each one has his or her self values and needs.
           But life is for living, living is interacting with these different people; every hour, every minute and every second. If you interact with them they have access to your life. Everyone wants to make you be how they want you to be. But the question is how should you be to please all those around you? Who should you listen to as to please all of them?
           Trying to please all of them is impossible; it is very far from being possible. Be yourself that’s the only way out. You are more important than anyone else around you. They can only advice but the effects of whatever they advice come directly to you; not to all those around you, no matter how close they are. Only you suffer the blow of what you do.
             I once asked myself; why didn’t God put only one brain so that we can all share it? Why do we get hurt individually and all together? Why?
What others want for you is not important for you, that is what they want not what God wants for you; not the reason why you were created, what you want for you is very important. It’s your mission in your life. It leads to your destination;                        YOUR DESTINATION, no one else YOURS ONLY.
             No one else has the power to make you fail unless you allow them to do so. We open the doors of our lives to them and they penetrate too much that we can’t even stand on what we want. What do we get when we fulfill the dreams of the world to us and fail to achieve our own goals.
              You have the powers to decide the extent to which people can interfere with your life and way of living. In your life you’re more important. Oxygen is for all of us but you breathe through your own nose; not through anyone’s nose; that shows in life you stand alone!
It is your fight not a TEAM WORK. You’re responsible for your life!!!
      Prepared by HEAVEN DAVID

PICHA YA AJALI ILITOKEA JANA,BASI LA BUNDA EXPRESS

Eneo la katikati ya Lugeye na Nyanguge basi la abiria la 'Bunda Express' lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea Mwanza muda wa saa mbili asubuhi jana lilipata ajali mbaya, mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na umauti na wengine kuwa majeruhi na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.
Eneo la magu basi la abiria la 'Bunda Express' lenye namba za usajili T 782 BKZ likitokea Musoma kuelekea Mwanza muda wa saa mbili asubuhi jana lilipata ajali mbaya, mazingira yanaonesha kuwa idadi kubwa ya watu wamekutwa na umauti na wengine kuwa majeruhi na mvua kubwa ilikuwa ikinyesha.