
Pakiti za Bangi kama inavyouzwa katika masoko mengine
Mwezi uliopita, Majimbo mawili nchini marekani yalipiga kura kuhalalisha , kudhibiti na kutoza kodi bangi.
Kutokana na matangazo ya kibiashara na sheria za
kudhibiti ulevi wa bangi wakati madereva wakiwa njiani , basi tunahoji
nini cha mno kinachosubiriwa?
Kura iliyopigwa tarehe sita mwezi
Novemba katika majimbo ya Colorado na Washington, bila shaka iliwatia
furaha watumiaji wa Bangi lakini polisi wengi walilala wakiwa na
wasiwasi si haba.
Na hatua hiyo ikaleta karibu malumbano kati ya
majimbo hayo mawili na serikali ya kitaifa, kwani bangi ingali
imeharamishwa chini ya sheria za kitaifa. Lakini kama ilivyo ada, kila
jimbo nchini Marekani liko huru kutunga sheria zake.
Marijuana kama inavyojulikana na wengi, ni dawa
ya kulevya inayotumiwa sana nchini Marekani. Lakini sasa wataalamu
wanasema huu ni mwanzo tu wa kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya ambayo
bado imepigwa marufuku.
“Hiki ni kionjo tu, bado mengi yatakuja’’ alisema Sanho Tree mkuregenzi mkuu wa mradi kuhusu sera ya mihadarati.
"Ikiwa majimbo haya mawili yataendelea na
harakati zao za kuhalalisha dawa hiyo ya kulevya, bila mawingu kuanguka,
basi utakuwa mwanzo mpya kwa uhuru wa kisiasa." Alisema Sanho
Lakini watawala wako macho
"Wakuu wa polisi mjini Colorado wana wasiwasi kuhusu usalama wa watu kwa ujumla" anasema afisaa mmoja wa polisi John Jackson

Kijana mdogo akivuta bangi wakati wa maandamano ya kutaka kuhalalishwa kwa bangi Marekani
Takriban miaka 80 baada ya Marekani kufutilia
mbali sheria iliyoharamisha pombe, tunajaribu kujibu baadhi ya maswali
ya watu walioelezea hisia mbali mbali kuhusu bangi kuhalalishwa.
Je wauzaji na wakulima wa Bangi wataendesha vipi matangazo ya kibiashara ya bangi?
Ni haramu kwa watu walio chini ya umri wa mia 21
kupatikana na bangi huku jimbo la Washington likiharamisha matangazo a
kibiashara ya bangi katika maeneo ya watoto kuchezea .
Kwa watu ambao hawajahi kutumia bangi , harufu
na aina zote za bangi ni sawa tu, wakati inapovutwa athari zake ni sawa
tu, yaani hakuna tofauti kubwa.
Wakati itakapohalalishwa, je wauzaji/makampuni
katika maeneo ya Washington na Colorado yataendesha vipi biashara zao
ili kupata wateja wengi?
“Iwe ni soksi au bangi, kitu cha kwanza mteja
atataka kufanya ni kuangalia muuzaji wa bidhaa ile.’’ Hii ni kulingana
na mtaalamu mmoja wa matangazo ya kibiashara mjini New York.
Anasema kuwa soko la bangi lipo lakini kama ni
kwa vijana wenye umri wa miaka ishirini na zaidi, ambao tayari
wanaitumia , hakuna ugumu hapo, kwani hawatahitaji matangazo ya
kuwashawishi ili kununua.
Kibarua ni kwa wahafidhina ambao labda kwa
sababu ya maadili, hawavuti bangi. Lakini soko linaweza kuwepo kwa
wataalamu wanaosongwa na mawazo au wapambe wa kiafya na kadhalika.
Muuzaji wa bangi anaweza kubuni mbinu ya kipekee
ya kuuza bangi na kuweza kuifunga kwenye pakiti za kuvutia kwa rangi na
ambazo zina mvuto wa kuwa ghali , labda ndio kitu kitakachoweza
kuwavutia wanunuaji.

Mjini Asmterdam Bangi hutumiwa kama kiungo katika baadhi ya vyakula kama keki hizi
Je mwajiri anaweza kukulazimisha kufanyiwa uchunguzi wa madawa ya kulevya?
Katika jimbo la Colorado, utumiaji wa Bangi bado
unaweza kukuweka mashakani, kwani, sheria hiyo mpya, inawaruhusu
waajiri kuharamisha utumiaji wa bangi miongoni mwa wafanyakazi.
"Hii haishurutishi mageuzi yoyote,’’ anasema
Mason Tvert, mmoja wa wanaharakati wanaotaka matumizi ya Bangi
kudhibitiwa kama ilivyo pombe katika jimbo la Colorado.
Sheria ya taifa nayo haina msimamo halisi kuhusu swala hili
Lakini uchunguzi uliokuwa unafanyiwa
wafanyafakazi kwenye maofisi umendelea kudidimia. Inahofiwa waajiri
katika majimbo ya Colorado na Washington, sasa watatupilia mbali jukumu
la kuhakikisha wafanyakazi maofisini hawaji kazini wakiwa walevi wa
bangi
Uchunguzi mwingi unaofanyiwa watu kubaini ikiwa
wanatumia mihadarati, ni kutokana na dhana kuwa wafanyakazi wengi
wanaotumia madawa hayo, huathiri biashara.
Wafanyakazi wengi wanaopatikana wakiwa na
chembechembe za mihadarati mwilini, wanajulikana kama 'wavutaji wa bangi
wa Jumamosi,' yaani waliovuta bangi mwishoni mwa wiki. Na hivyo
hawawezi kufanya kazi.
Sheria za marekani wakati mmoja ziliharamisha pombe. Je sheria hizi zinaashiria kuwa nchi hiyo iko tayari kuhalalisha bangi?

Mimea ya Bangi
Majimbo mawili nayo tayari yamegusia uwezekano wa kuwasilisha mswaada wa kuhalalisha Bangi.
Baadhi ya watu hutumia Bangi kama njia ya
kujiliwaza, kujiburudisha au wakiwa waraibu. Wengine wanasisitiza kuwa
Bangi inafaida za kimatibabu.
Nini maoni yako kuhusu swala hili tete?