Thursday, January 24, 2013

WANAFUNZI WA ST JOHN DODOMA ZAIDI YA 5000 WAMENDAMANA KATIKATI YA MJI WA DODOMA WAKIPINGA UBAKAJI NA ULAWITI:

Wanafunzi wa Saint John University wakiwa wamebeba mabango katika maandamano yaliyofanywa leo
Hivi ndivo ilivyokuwa katika mji wa Dodoma kufuatia maandamano  wanafunzi wa Saint John University

Hayo ndiyo yalikuwa ya moyoni mwa wanafunzi wa chuo cha Saint John Dodoma



 
        W anafunzi zaidi ya 5000 wa chuo cha Saint John Dodoma wameandamana leo kushinikiza Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma liwajibike katika matukio ya kiuhalifu yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yakiwemo mauaji yanayofanywa na vibaka na majambazi.
         Maandamano hayo yamefanywa kutokana na kudaiwa na wanafunzi hao kuwa kumekuwa hakuna uwajibikaji wa Jeshi la Polisi katika usalama wao.
          Jumatatu ya wiki hii nikimaanisha Tarehe 21 / January / 2013 mwanachuo aliuawa na kuporwa simu,siku ya jana katika Hosteli za akina dada zilivamiwa Laptop , simu na fedha ziliporwa, katika tukio hilo la jana wanfunzi walipigwa na kujeruhiwa vibaya.
           Mkuu wa polisi mkoa wa Dodoma ameahidi kulifanyia kazi tatizo hilo na kuimarisha ulinzi chuoni hapo.

ULINZI WAIMALISHWA KWA WANAFUNZI WA IFM BAADA YA KASHFA YA UBAKAJI NA KUIBIWA NA VIBAKA



UONGOZI wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha Usimamazi wa Fedha (IFMSO) cha jijini Dar es Salaam, umesema hali ya usalama kwa sasa katika Hosteli za Kigamboni inaridhisha.
Waziri Mkuu wa IFMSO, Daniel Sarungi alisema jana kuwa tangu iundwe timu ya polisi inayoshirikiana na wanafunzi hao hali imekuwa tulivu kwa kipindi cha wiki moja iliyopita. 
Sarungi alisema kuwa hakujatokea uvamizi tena katika hosteli zao, lakini akaongeza kusema kuwa taarifa kamili ya ripoti ya timu hiyo itatolewa na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova.
“Kuna amani sana, misako imefanyika lakini ripoti itatolewa Januari 30 na Kamanda Kova,” alisema Sarungi.
Kauli ya Kiongozi huyo wa wanafunzi haikutofautina na ya Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Englbert Kiondo, ambaye alisema taarifa inayohusu hali ilivyo itatolewa na Kamanda Kova.

Kwa upande wa wakazi wa Kigamboni, walisema kuwa wameshuhudia polisi wakifanya doria maeneo hayo tofauti na ilivyokuwa huko nyuma kabla wanafunzi hawajaandamana.
Walisema pia wameona polisi wakiwakamata wahalifu kwenye maeneo hayo kutokana na misako wanayoifanya hali ambayo imeleta utulivu kwenye mji huo.
“Kwa sasa kumetulia inawezekana wanasikilizia (wahalifu), likini ingetakiwa polisi wawakamate wale vinara kwa sababu wanawafahamu” alisema Salum Rashid mkazi wa eneo hilo.
Naye mkazi mwingine anayejishughulisha na biashara ya kioski, alisema kuwa kumekuwa na utulivu kwani hata wanafunzi ambao ndiyo wateja wake wakubwa wanamwambia kuwa wanaweza kuacha vitu wakavikuta salama.

Mkasi - SO3E09 with Hasheem Thabeet ( JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA )

NEW VIDEO : SEMINDE FT MUBBYZOW - BATA

WANANCHI WAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUCHOMA NYUMBA ZAO


Habari iliyotufikia hivi punde inaeleza kuwa kundi kubwa la wananchi waliojawa na ghazabu Wilayani Rufiji leo wamevamia kituo cha Polisi Kibiti Wilayani humo na kuanzisha vurugu kubwa kufuatia raia mmoja mkazi wa kijiji hicho kudaiwa kufa kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kutokana na kipigo cha Polisi.

Chanzo chetu cha Habari kutoka Kibiti kinatupasha kuwa,kijana huyo aliyefariki kutokana na kipigo hicho afahamikae kwa jina la Hamis Mpondi ambaye mauti yamemfika wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,jijini Dar es Salaam na taarifa hiyo ilipowafikia wananchi hao ndipo wakachukua uamuzi wa kwenda kituoni hapo na kuanzisha vurugu hizo.

Habari zaidi zinaeleza kuwa,hivi sasa wananchi hao wanateketeza nyumba za Askari Polisi hao zilizopo jirani kabisa na kituo hicho, licha ya juhudi za Polisi kuwatawanya kwa mabomu kuendelea kufanyika.

Aidha wananchi hao wameanza kufunga barabara kuu ya Kilwa iendayo Mikoa ya Kusini, Lindi na Mtwara kwa mawe, magogo na kuchoma matairi ikiwa ni umbali wa kama kilometa moja kutoka kituo cha Polisi Kibiti.

Inaelezwa kuwa hali imezidi kuwa tete katika eneo hilo huku Polisi wa Kibiti wakiendelea na jitihada za kudhibiti hali hiyo kwa kufyatua mabomu ya machozi hewani kujaribu kutawanya umati huo wa watu.

tutaendelea kupeana taarifa zaidi kadri zitakavyokuwa zikitufikia.

NEW TRACK : NOORAH aka BABA STYLZ ft ALI KIBA -NIKUPE NINI

KEISHA FT DIAMOND - NIMECHOKA ( OFFICIAL VIDEO )

NEW VIDEO: 50 Cent ft. Snoop & Young Jeezy - Major Distribution

NEW TRACK : NAY WA MITEGO - UTAVUNA ULICHOPANDA

SHINE RECORDS .....TUNA PENDA KUTANGULIZA SHUKRANI ZETU KWA WOTE AMBAO MNATUJALI KWA MAMBO MENGI AMBAYO TUNAFANYA NA PIA TUNAPENDA KUOMBA MSAMAHA KWA WOTE AMBAO TULIWAKERA NA KUTUHISI TUNAWADHARAU NA TUNAPENDA KUTAMBULISHA NGOMA MPYA YA MSANII ..NEY WAMITEGO AMBAYO INA KWENDA NA UJUMBE WA UTAVUNAULICHOPANDA........IKIWA IMEFANYIKA ....SHINE RECORDS.....,,,,CHINI YA MR T....