Thursday, January 24, 2013

WANAFUNZI WA ST JOHN DODOMA ZAIDI YA 5000 WAMENDAMANA KATIKATI YA MJI WA DODOMA WAKIPINGA UBAKAJI NA ULAWITI:

Wanafunzi wa Saint John University wakiwa wamebeba mabango katika maandamano yaliyofanywa leo
Hivi ndivo ilivyokuwa katika mji wa Dodoma kufuatia maandamano  wanafunzi wa Saint John University

Hayo ndiyo yalikuwa ya moyoni mwa wanafunzi wa chuo cha Saint John Dodoma



 
        W anafunzi zaidi ya 5000 wa chuo cha Saint John Dodoma wameandamana leo kushinikiza Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma liwajibike katika matukio ya kiuhalifu yanayoendelea kutokea ndani ya chuo yakiwemo mauaji yanayofanywa na vibaka na majambazi.
         Maandamano hayo yamefanywa kutokana na kudaiwa na wanafunzi hao kuwa kumekuwa hakuna uwajibikaji wa Jeshi la Polisi katika usalama wao.
          Jumatatu ya wiki hii nikimaanisha Tarehe 21 / January / 2013 mwanachuo aliuawa na kuporwa simu,siku ya jana katika Hosteli za akina dada zilivamiwa Laptop , simu na fedha ziliporwa, katika tukio hilo la jana wanfunzi walipigwa na kujeruhiwa vibaya.
           Mkuu wa polisi mkoa wa Dodoma ameahidi kulifanyia kazi tatizo hilo na kuimarisha ulinzi chuoni hapo.

No comments:

Post a Comment