Tuesday, January 15, 2013

NEW TRACK: MONSTAR - SIJAWASUSA (VUMILIA)

Artist: MONSTAR
Song: SIJAWASUSA (VUMILIA)
Studio: EXPENSIVE MUSIC
Producer: ZIDADAY MWAMBA

HUYU NDIO MWIZI ALIEIBA VITU KWENYE GARI LA MSANII MH TEMBA

Kwa mara ya kwanza juzi january 10 2013 ndio zilitangazwa habari za msanii Mh Temba kuibiwa vitu vya gari lake kwa mara ya tano, amekua na magari tofauti tofauti ambapo kwa mara tano ameibiwa vitu mbalimbali ambapo baadae amekua akilazimika kununua vitu vilevile vya kwake.
Hizi picha amezituma Exclusive kwa millardayo.com na kusema huyu jamaa anatuhumiwa kuwa mwizi hodari wa power window, vioo na vifaa vingine vya magari mbalimbali ambapo alipohojiwa na polisi amesema yeye huwa ananunua tu vifaa vya magari lakini hausiki kufanya wizi.

Wanaofanya wizi ni wengine ndio wanamletea na yeye anafanya kazi ya kumpigia simu mwenye mali ili aje avinunue vifaa vilivyoibiwa kwenye gari lake, sasa kilichofanya Mh Temba amkamate ni pale alipopigiwa simu na huyu huyu jamaa na kudai kwamba anavyo vifaa vilivyoibwa kwenye gari lake.
.

                                                 Hii ndio Verosa ambayo waliiba vifaa ambavyo baadae Temba alikuja kuvinunua kwa laki nane, na ni vifaa vilevile vilivyoibwa kwenye gari lake.
Kumbe huyu jamaa ndio yule yule aliwahi kumpigia simu Temba wakati alipoibiwa tena vifaa vya gari november 2012 na kumuuzia vifaa vilevile kwa shilingi laki nane huku Temba akiitoa hiyo pesa akiwa anajua kabisa vifaa anavyonunua ni vilevile, wakati huu Temba bado alikua ameisave namba yake kwa hiyo akashtukia mchezo kwamba jamaa ndio wanamchezea hivyo akajipanga na kwenda kumkamata.

Mtuhumiwa alipofikishwa polisi akajitetea kwamba yeye hausiki na wizi, yeye anafanya udalali wa kununua na kuuza hivyo vifaa tu na wala vitu vingine vinavyoibwa kwenye magari kama Camera na Laptop huwa hausiki navyo na wala havinunui.
Polisi wanamjua kabisa na namba yake wanayo kwa sababu jamaa amekua na kesi hizo mara nyingi sana hapo kituoni, mara ya mwisho ambapo wengi wanaoibiwa vifaa huwa anawaambia watume pesa kupitia line yake ya simu ya mkononi alafu wakishatuma ndio mtu anatumwa kwenda kuvipeleka hivyo vifaa, kama alivyofanya kwa Mh Temba mara ya mwisho na alitaka kufanya hivyo hata wakati huu.

Mh Temba amerudishiwa vifaa vyake alivyoibiwa wakati huu na mtuhumiwa ameachiwa, sio kwa dhamana ila wamechukua tu alama zake za vidole wakamwambia arudi jumatatu, Temba nae kaambiwa arudi jumatatu.

ALA KICHAPO BAADA YA KUNASWA AKILWAWITI WATOTO WADOGO:


Mwananchi huyu mwenye hasira kali akimnyanyua juu kibaka huyo na kumtupa chini kama akina 'John Cena'.
..Kichapo kikiendelea kwa kibaka huyo.
Kibaka huyo akizidi kuhukumiwa mtaani.
Ustadhi akijaribu kumnusuru kibaka huyo.
Ustadhi huyo aliamua kuondoka na kibaka ili kumwokoa.
Akimpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani.
KIJANA mmoja anayesadikiwa kuwa ni kibaka mchana huu amenusurika kifo baada ya kupokea kichapo kikali kutoka kwa wananachi wenye hasira wakimshutumu kuiba watoto wadogo na kwenda nao eneo la mto Morogoro chini ya daraja la Shani na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
Akizungumza na Mtandao huu mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Juma Athuman alidai kwamba kijana huyo ana kawaida ya kuwateka watoto wadogo hasa wa shule na kuwapeleka chini ya daraja hilo na kuwafanyia vitendo vya kihuni.
" Kwa kipindi kirefu tulikuwa tukimsaka kibaka huyu ambaye ana tabia ya kuwateka watoto wadogo na kuwapeleka mto wa Morogoro chini ya daraja la Shani.
"Muda huu tumemfuma akiwa chini ya daraja hilo na mtoto mdogo ndipo tulipomfukuza na kufanikiwa kumkamata eneo hili la kituo cha mafuta jirani na daraja hili la Shani," alisema Juma Athuman.
Katika hatua nyingine 'ustadhi' mmoja alijitosa na kumnyakua kibaka huyo kutoka mikononi mwa kundi la wananchi hao na kumpeleka kituo kikuu cha polisi kilichopo jirani na eneo hilo la Shani SOURCE:
 

MATUKIO YA WANAFUNZI WA IFM WALIVYOCHEZEA KICHAPO KUTOKA KWA POLISI:



BAADA ya wanafunzi wa Chuo Cha Uongozi wa Fedha (IFM) kwenda kigamboni ambako Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova kuwataka wakawasilishe hoja zao hukohuko ambako wanadai walipeleka majina ya wahalifu na hayajashughulikiwa, waligoma kufanya mkutano kwenye viwanja vya mpira eneo la Machava nakutaka mkutano huo ufanyike kwenye kituo cha polisi Cha Kigamboni ambako wanafunzi wengi wao walielekea huko.

VILIO NA KICHAPO TOKA KWA POLISI VILITAWALA MAANDAMANO YA YA WANAFUNZI WA IFM


Mwanafunzi aliyeshikwa akipandishwa kwenye Difenda.
Utakwenda Tu!


Mara baada ya kufika kwenye kituo hicho waliamriwa maratatu waondoke waende kwenye mkutano na Kamanda Kova wakakataa baada ya hapo ndipo mabomu yakaanza kupigwa. Kwenye mabomu hayo wanafunzi kadhaa walijeruhiwa na kuumia wengine walipoteza fahamu.

Hata hivyo walioshikiliwa wote waliachiwa na kutakiwa kwenda kwenye mkutano huo ambao uliazimia mambo kadhaa ya utekelezaji ili kutatua tatizo hilo la wizi kwenye eneo hilo. Kamanda Kova aliwaahidi wanafunzi hao kuwa watapata mrejesho wa hatua walizochukuwa siku ya tarehe 30 mwezi huu