![]() |
Kwa mara ya kwanza juzi january
10 2013 ndio zilitangazwa habari za msanii Mh Temba kuibiwa vitu vya
gari lake kwa mara ya tano, amekua na magari tofauti tofauti ambapo kwa
mara tano ameibiwa vitu mbalimbali ambapo baadae amekua akilazimika
kununua vitu vilevile vya kwake. Hizi picha amezituma Exclusive kwa millardayo.com na kusema huyu jamaa anatuhumiwa kuwa mwizi hodari wa power window, vioo na vifaa vingine vya magari mbalimbali ambapo alipohojiwa na polisi amesema yeye huwa ananunua tu vifaa vya magari lakini hausiki kufanya wizi. Wanaofanya wizi ni wengine ndio wanamletea na yeye anafanya kazi ya kumpigia simu mwenye mali ili aje avinunue vifaa vilivyoibiwa kwenye gari lake, sasa kilichofanya Mh Temba amkamate ni pale alipopigiwa simu na huyu huyu jamaa na kudai kwamba anavyo vifaa vilivyoibwa kwenye gari lake. |
.
![]() |
Hii
ndio Verosa ambayo waliiba vifaa ambavyo baadae Temba alikuja kuvinunua
kwa laki nane, na ni vifaa vilevile vilivyoibwa kwenye gari lake.
Kumbe huyu jamaa ndio yule yule
aliwahi kumpigia simu Temba wakati alipoibiwa tena vifaa vya gari
november 2012 na kumuuzia vifaa vilevile kwa shilingi laki nane huku
Temba akiitoa hiyo pesa akiwa anajua kabisa vifaa anavyonunua ni
vilevile, wakati huu Temba bado alikua ameisave namba yake kwa hiyo
akashtukia mchezo kwamba jamaa ndio wanamchezea hivyo akajipanga na
kwenda kumkamata.
|
![]() |
Mtuhumiwa alipofikishwa polisi
akajitetea kwamba yeye hausiki na wizi, yeye anafanya udalali wa kununua
na kuuza hivyo vifaa tu na wala vitu vingine vinavyoibwa kwenye magari
kama Camera na Laptop huwa hausiki navyo na wala havinunui.
Polisi wanamjua kabisa na namba yake wanayo kwa sababu jamaa amekua na kesi hizo mara nyingi sana hapo kituoni, mara ya mwisho ambapo wengi wanaoibiwa vifaa huwa anawaambia watume pesa kupitia line yake ya simu ya mkononi alafu wakishatuma ndio mtu anatumwa kwenda kuvipeleka hivyo vifaa, kama alivyofanya kwa Mh Temba mara ya mwisho na alitaka kufanya hivyo hata wakati huu. Mh Temba amerudishiwa vifaa vyake alivyoibiwa wakati huu na mtuhumiwa ameachiwa, sio kwa dhamana ila wamechukua tu alama zake za vidole wakamwambia arudi jumatatu, Temba nae kaambiwa arudi jumatatu. |
No comments:
Post a Comment