MADOLE
PATA HABARI NA BURUDIKA
Tuesday, January 22, 2013
SAKATA LA KAHABA ALIYEOKOKA......
Mwanamke
huyu alijitambua vyema na kukiri ndani ya nafsi yake kuwa hawezi
kuolewa na mwanaume yoyote yule maana jamii yote ilikuwa inamtambua
kwa uchangudoa wake......
Kwa
hiyo , ili kurahisisha mambo na kuifanya biashara yake iimarike,
mwanadada huyu aliamua kwenda hospitali kukitoa kizazi
chake.Hakutaka tena usumbufu wa kutoa mimba au kufikiria
kondomu......
Tangu wakati ule biashara yake iliimarika na wateja walizidi kumiminika.Baada ya miaka
kadhaa, Upako wa mwenyezi mungu ulimfikia kupitia kwa mtumishi
mmoja wa mungu ambaye alifanikiwa kumfanya aokoke na kuwa
mtumishi mzuri kanisani.....
Siku moja, mchungaji mmoja alimwita na kumwambia kuwa:
"Dada yangu, Mwenyezi mungu amenena na mimi na kunifunulia kuwa wewe ndo mke wangu wa ndoa, hivyo naomba tuoane.."
Mwanamke huyu alitabasamu na kusema:
"Kaka
yangu, Mungu hajakwambia lolote, lasivyo, utakuwa hujamsikia
vizuri.Naomba uniache tu maana sina mpango wowote wa kuolewa"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Yule mchungaji aliendelea kushikilia msimamo wake na kudai kuwa :
"Mungu amenifunulia,wewe ndo mke wangu"
Mwanamke huyu aliendelea kuyapuuza maneno hayo na ndipo sakata hilo lilipomfikia Askofu wa kanisa hilo.....
Wakiwa mbele ya mchungaji,Mwanamke huyu alifunguka kwa uwazi mbele ya askofu na kudai kuwa kabla ya kuokoka yeye alikuwa ni kahaba wa makahaba....
Askofu naye alifunguka na kudai kuwa :"Sioni sababu ya kuumiza kichwa kwa mambo yaliyopita.Mungu humsamehe mwanadamu kwa kuzifuta dhambi zake zote za nyuma na kumfanya awe mpya..!!!"
Mwanamke huyu alifunguka tena na kudai kuwa:
"Baba askofu, mimi nilishatoa kizazi changu wakati nikiwa kahaba, kwa hiyo sitaweza kuzaa tena"
Askofu aliishiwa pumzi baada ya kusikia hivyo.Hakuweza tena kusema kuhusu kusahau ya nyuma.Ilibidi amgeukie yule mchungaji na kumwamba:
"Vipi, bado kuna maono yoyote toka kwa mwenyezi mungu?"
Mchungaji alijibu ,"Ndio, huyu ndo mke wangu.."
Askofu ilibidi awaombee kwa sala maalumu.Hatimaye ndoa ikafungwa......Baada ya miezi michache tu, huyu mwanamke alibeba mimba.Yeye pamoja na mumewe waliongozana pamoja kwenda hospitalini, tena kwa yule yule doctor aliyekitoa kile kizazi......
Daktari alipomuona alifurahi akidhani kuwa pengine mteja wake kamletea mteja mwingine.....Doctor hakuamini masikio yake baada ya kuambiwa kuwa huyu mwanamke ni mjamzito na amekuja kujiandikisha clinic....
Hakika Mungu ni Muweza wa yote....
SOURCE;MPEKUZI
MWANACHUO WA SAINT JOHN, DODOMA AUAWA KIKATILI
JESHI la
polisi mkoani Dodoma limeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi
katika baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa
kinyama kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na
watu wasiojulikana.
Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya jumapili hii majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho chenye wanafunzi 5500 akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.
Ni simanzi,vilio,huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.
Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda wanadai kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa kunyofolewa macho,masikio,pua,mguu na viuno vingine.
Prof.Gabriel Mwaluko ni makamu mkuu wa Chuo na Karimu Meshack ni afisa habari ambao kwa pamoja wanaelezea kilichorjiri.
Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo, Kamanda wa mkoa ACP David Misime anawataka wakazi wa mkoa huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.
Wakati huo huo Kamanda Misime anasema msako mkali umeanza wa kuwatia nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono ya sheria kwa ajili ya hukumu.
Subscribe to:
Posts (Atom)