Showing posts with label MUSIC. Show all posts
Showing posts with label MUSIC. Show all posts

Saturday, January 19, 2013

Teaser: Kaa tayari kwa video ya 'Ki-utu Uzima' by Joh Makini...Coming soon.

Mwamba wa kaskazini mweusi Joh Makini ametoa ishara, soon atawasha 'green light'. Kaa tayari kuipokea video yake mpya ya Ki-Utu Uzima, cooming soon.

Teaser: Mwana Fa - The Finest


Mwana Fa a.k.a Binamu ametease picha hii kupitia akaunti yake ya Instagram, so ni miongoni mwa new joints zinazotegemewa kutoka hivi karibuni.

NEW TRACK : AINEA ft SHETA - SOMEBODY

                                PROUCTION : ECK PRODUCTION
                                PRODUCER :   ECK

Friday, January 18, 2013

NEW TRACK : JACO BEATS - LOVE IS


                                          SONG : LOVE IS
                                          MSANII : JACO BEATS
                                          PRODUCTION : LONG MILES
                                          PRODUCER : JACO BEATS
   Jaco Beats ni moja ya wasanii wanaofanya vizuri katika industry ya mziki Tanzania. Anafanya vizuri akiwa msanii huku Producer,Mziki wake anaufanya pande za Dodoma.
 

Wednesday, January 16, 2013

New Song: Pnc, Z-Anto, Dogo Janja, Pingu & Cassim - Mtu wa Watu

Artists: PNC, Z-ANTO, DOGO JANJA, PINGU & CASSIM MGANGA
Song: MTU WA WATU

NEW TRACK; SAJNA ft BELLE 9 & PIPI-ROHO MBAYA (PRODUCED BY DUKE)

Baada ya kipindi kirefu kupita msanii Faraji Twaha a.k.a Sajna ameamua kuachia wimbo wake unaoitwa 'ROHO MBAYA' ambao aliurekodi takribani miaka miwili iliyopita na kuwashirikisha Belle 9 pamoja na mwanadada Pipi.
Kwa mujibu wa Sajna wimbo huu sio official single yake ya mwaka huu lakini ameutoa kuvunja ukimya uliotokana na kubanwa na shule na pia kama zawadi kwa fans wake, wakati anajiandaa kutoa official song yake ya mwaka huu 2013. Roho mbaya pia inapatikana katika album yake ya kwanza inayoitwa Iveta.

Tuesday, January 15, 2013

NEW TRACK: MONSTAR - SIJAWASUSA (VUMILIA)

Artist: MONSTAR
Song: SIJAWASUSA (VUMILIA)
Studio: EXPENSIVE MUSIC
Producer: ZIDADAY MWAMBA

HUYU NDIO MWIZI ALIEIBA VITU KWENYE GARI LA MSANII MH TEMBA

Kwa mara ya kwanza juzi january 10 2013 ndio zilitangazwa habari za msanii Mh Temba kuibiwa vitu vya gari lake kwa mara ya tano, amekua na magari tofauti tofauti ambapo kwa mara tano ameibiwa vitu mbalimbali ambapo baadae amekua akilazimika kununua vitu vilevile vya kwake.
Hizi picha amezituma Exclusive kwa millardayo.com na kusema huyu jamaa anatuhumiwa kuwa mwizi hodari wa power window, vioo na vifaa vingine vya magari mbalimbali ambapo alipohojiwa na polisi amesema yeye huwa ananunua tu vifaa vya magari lakini hausiki kufanya wizi.

Wanaofanya wizi ni wengine ndio wanamletea na yeye anafanya kazi ya kumpigia simu mwenye mali ili aje avinunue vifaa vilivyoibiwa kwenye gari lake, sasa kilichofanya Mh Temba amkamate ni pale alipopigiwa simu na huyu huyu jamaa na kudai kwamba anavyo vifaa vilivyoibwa kwenye gari lake.
.

                                                 Hii ndio Verosa ambayo waliiba vifaa ambavyo baadae Temba alikuja kuvinunua kwa laki nane, na ni vifaa vilevile vilivyoibwa kwenye gari lake.
Kumbe huyu jamaa ndio yule yule aliwahi kumpigia simu Temba wakati alipoibiwa tena vifaa vya gari november 2012 na kumuuzia vifaa vilevile kwa shilingi laki nane huku Temba akiitoa hiyo pesa akiwa anajua kabisa vifaa anavyonunua ni vilevile, wakati huu Temba bado alikua ameisave namba yake kwa hiyo akashtukia mchezo kwamba jamaa ndio wanamchezea hivyo akajipanga na kwenda kumkamata.

Mtuhumiwa alipofikishwa polisi akajitetea kwamba yeye hausiki na wizi, yeye anafanya udalali wa kununua na kuuza hivyo vifaa tu na wala vitu vingine vinavyoibwa kwenye magari kama Camera na Laptop huwa hausiki navyo na wala havinunui.
Polisi wanamjua kabisa na namba yake wanayo kwa sababu jamaa amekua na kesi hizo mara nyingi sana hapo kituoni, mara ya mwisho ambapo wengi wanaoibiwa vifaa huwa anawaambia watume pesa kupitia line yake ya simu ya mkononi alafu wakishatuma ndio mtu anatumwa kwenda kuvipeleka hivyo vifaa, kama alivyofanya kwa Mh Temba mara ya mwisho na alitaka kufanya hivyo hata wakati huu.

Mh Temba amerudishiwa vifaa vyake alivyoibiwa wakati huu na mtuhumiwa ameachiwa, sio kwa dhamana ila wamechukua tu alama zake za vidole wakamwambia arudi jumatatu, Temba nae kaambiwa arudi jumatatu.

Sunday, January 13, 2013

NEW TRACK-Gusher-Bado wewe

Kutana na Msanii Chipukizi "Gusher" anayekuja na crunk aloita "Bado wewe" ikiwa imewalenga viongozi walopotosha maana nzima ya uongozi bora nchini,Kijana Gusher toka panda za kaskazini mwa Tanzania amerekodi pini pande za noizmekah,ni mwenye juhudi na malengo makubwa katika kuonyesha kipaji chake anaomba support yenu mashabiki na wadau kwa ujumla, kupata kuisikiliza nyimbo hii ya "BADO

NEW TRACK-ManBatoo-She nah Leave(NOIZ)

Pata brand new riddim toka kwa ManBatoo aka Rudbwai from Arachuga Kijenge juu,Reggae joint inakwenda kwa jina "She nah leave" ikiwa ni new years release juu ya "heart & soul riddim" na mixing pande za www.noizmekah.com.

PSY-Gngnam Style Mash-Up

Tuesday, December 25, 2012

Wanawake marufuku kuvaa nguo fupi




Wanawake wa Swaziland
Wanawake nchini Swaziland wako katika hatari ya kukamatwa na polisi iwapo watavaa sketi fupi au blauzi ambazo zitaonyesha tumbo likiwa wazi.
Msemaji wa polisi Wendy Hleta amesema polisi watatekeleza sheria ya mwaka1889 ambayo inapiga marufuku uvaaji wa nguo zinazokosa maadili.
Msemaji huyo wa polisi pia amesema wanawake wanaovaa nguo fupi ni kivutio cha wabakaji.
Hata hivyo, sheria hiyo ya kikoloni haitumiki katika uvaaji wa nguo za kijadi ambazo zinavaliwa na wanawake, sehemu kubwa ya miili yao inaachwa wazi.
Mavazi hayo huvaliwa wakati wa sherehe, zikiwemo za mwaka zinazompa Mfalme fursa ya kuchagua mke wake mpya.
Mwaka 2000, serikali ilitunga sheria inayowataka wanafunzi wa kike kuanzia miaka 10 na zaidi kuvaa sketi zinazovuka magoti kama njia ya kuwalinda dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Mfalme Mswati III wa Swaziland

Swaziland ina idadi ya watu milioni1.2 na moja kati ya nchi zenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya ukimwi duniani.


Bi Hleta amesema sheria hiyo ya mwaka1889 haijaweza kutekelezwa katika miaka ya karibuni.

Amesema polisi wanataka kuwajulisha wanawake kuwa sheria hiyo bado ipo na inafanya kazi.
Baadhi ya wanaume katika mji wa Manzini wamesemekana kuwalalamikia wanawake wanaovaa kuvaa nguo fupi.
source:BBC