Friday, December 7, 2012

KILIMANJARO STARS YATOLEWA CECAFA

Thursday, December 06, 2012 11:58 PM
Timu ya Tanzania bara (Kilimanjaro stars) imekubali kichapo cha aibu cha mabao 3-0 dhidi ya wenyeji wake Uganda katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Tusker Challenge. Timu ya taifa Tanzania bara (Kilimanjaro Stars)imefuta matumaini ya yake ya kurejea nchini na kome la challenge, baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Uganda, ambao ndiyo wenyeji wa mashindano hayo mwaka huu, Uganda waliandika bao la kwanza kupitia kiungo wao machachali Emmanuel Okwi katika dakika ya 11, bao hilo liliendelea mpaka timu hizo zinakwenda mapunziko.

baada ya mapunziko timu ya Uganda ilirejea uwanjani na kasi ya ajabu na kuweza kuandika bao la pili kupitia mshambuliaje wao Robert Ssentongo katika dakika ya 51, hali ilizidi kuwa mbaya kwa upande wa Stars na ilipofika dakika ya 71 Ssentongo alishindilia msumari wa mwisho kwa Stars na kuwezesha timu yake itoke kifua mbele kwa ushindi wa mabao 3-0.

Mechi hiyo ilicheza katika Uwanja wa Mandela, Namboole mjini Kampala, na kwa matokeo hayo,

timu ya taifa Tanzania bara itacheza na timu ya Zanzibar katika mchezo wa kumsaka mshindi wa tatu, wakati fainali itachezwa na timu ya taifa ya Kenya na Uganda.