

Wachrezaji
wa timu ya Yanga wakishangilia mara baada ya kufunga goli la kwanza
katika mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini.

Mashabiki wa Yanga wakishangilia wakati timu yao ikicheza kwenye uwanja wa Taifa jioni hii.

Kikosi cha timu ya Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Mchezaji
wa timu ya Yanga Kabange Twite akimiliki mpira mbele ya Nkosiabo
Xakane mchezaji wa Black Leopards ya Afrika Kusini .katika mchezo wa
kirafiki uliokutanisha timu hizo kwenye uwanja wa Taifa jioni hii, timu
ya Yanga imeshinda magoli 3-2 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini.
Goli la Yanga limefungwa na
mchezaji Jerrison Tegete kwa penati katika kipindi cha kwanza baada ya
Mchezaji Haruna Niyonzima kuangushwa katika eneo la hatari na mchezaji
wa timu ya Black Leopards na kuongeza goli la tatu katika kipindi cha
pili , Huku mchezaji Didier Kavumbagu akapachika goli la pili katika
kipindi katika kipindi hichohicho cha pili cha mchezo.
Timu ya Black Leopards ya Afrika
Kusini imefanikiwa kupata magoli mawili katika kipindi cha pili na
kufanya matokeo kuwa Yanga 3 na timu ya Black Leopards 2 mpaka mwisho wa
mchezao huo.
No comments:
Post a Comment