MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ametaka Katiba ijayo
ivipe mamlaka kamili vyombo vya uamuzi kwa lengo la kuviwezesha kufanya
kazi kwa uhuru pasipo kuingiliwa na mamlaka zingine.
Mnyika alitoa maoni hayo jana wakati akichangia mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya katika mkutano uliofanyika kwenye kata ya Makurumla, jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kutaka uhuru kwa baadhi ya taasisi, pia Mnyika alitaka Katiba mpya ieleze wazi kuhusu haki ya kupata elimu, kumiliki uchumi wa nchi kwa wananchi na upatikianaji wa maji ya uhakika ni haki inayoweza kudaiwa mahakamani.
Alisema Katiba ijayo iwawezeshe wananchi kuwatimua viongozi wa ngazi ya udiwani na ubunge ikiwa wataenda kinyume na matarajio ya uwepo wao madarakani.
Alivitaja vyombo ambavyo vinapaswa kuwa huru kuwa ni pamoja Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mwendesha Mashataka (DPP) na maeneo mengine ya uamuzi kama Bunge akisema kwa sasa havina uhuru wa kutosha wa kufanya kazi pasipo kuingiliwa na muhimili mwingine.
“Leo hii wabunge tukijidai kukataa bajeti ya serikali, Rais anaweza kulivunja Bunge na yeye akabakia na urais wake; hili suala lazima liangaliwe kwa umakini katika Katiba ijayo. Tusitoe nafasi ya kumfanya mtu mmoja kuwa na nguvu zilizopitiliza,” alisema Mnyika.
Alisema kwa taasisi kama TAKUKURU, DPP na zingine za Kikatiba ni lazima wanaopata fursa ya kufanya kazi waingie kwa sifa za kuomba badala ya kuteuliwa na Rais hali inayowafanya wasiwe na uwezo wa kuhoji sehemu yenye kuhisiwa kuwa na maslahi na uongozi wa juu wa nchi.
Katika kudhibiti ufisadi na kuongeza uwajibikaji, Mnyika alitaka Katiba mpya ihimize upendo na uwe msingi mkuu wa uwajibikaji kwa kila anayepata fursa ya kuwatumikia wananchi katika ngazi yoyote.
Katika utoaji wa maoni hayo Mnyika alionyesha wasiwasi wake wa kupatikana Katiba ya wananchi kwa kile alichoeleza kuwa watakaopitia maoni ya wananchi ni tume ileile iliyoteuliwa na mtu mmoja.
Alitaka tume ya sasa ya kukusanya maoni iandae ripoti ya mapendekezo na marekebisho maalumu na kuwa kuwe na tume huru itakayosimamia maoni ya wananchi yanayokusanywa.
Katika utoaji huo wa maoni, baadhi ya wananchi walitaka nafasi ya wakuu wa wilaya na mikoa kama kuna haja ya kuwepo ziwe ni za kupigiwa kura tofauti na zilivyo sasa ambapo wahusika huteuliwa.
Mapema asubuhi, tume hiyo ilikusanya maoni kwa wakazi wa Makuburi na Mabibo ambapo walipendekeza kuwa Katiba mpya izuie uwepo wa shule na hospitali za watu binafsi.
Mbele ya mjumbe wa tume hiyo, Ester Mkwizu, mwananchi mmoja Abbas Benard alisema kuwa uwepo wa shule na hospitali za watu binafsi unaongeza matabaka katika jamii na kuzidi kukandamiza watu wa hali ya chini.
Alisema kuwa viongozi na familia zao wanatibiwa kwenye hospitali binafsi na kuacha hospitali za serikali zikiwa hazina dawa, kitu ambacho kiko hata kwenye elimu.
“Shule za serikali hazina walimu na hazina vitabu, kwa hali hii mtoto wa maskini atajikomboa kweli?” alihoji Benard.
Alipendekeza mahakama kumchagua Jaji Mkuu badala ya kuteuliwa na Rais ambaye anateuwa viongozi wengi kulingana na mamlaka aliyokuwa nayo.
Naye Masoud Kaftany, alisema kuwa Katiba ya sasa iendelee kutumika, lakini baadhi ya vitu inabidi viongezwe na vingine vipunguzwe.
Kaftany alisema kuwa anapendekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40 hadi 65 wakati umri wa kugombea ubunge uwe kuanzia miaka 21 hadi 55, tofauti na ilivyokuwa katika Katiba ya zamani.
Alipendekeza kutolewa kwa viti maalumu vya wabunge na kupunguzwa kwa vyama vingi, vibakie vitatu ili kuzuia matumizi makubwa ya ruzuku ya serikali katika vyama hivyo.
Naye Harieth Raphael, alipendekeza kuwe na marekebisho ya sheria kandamizi hasa dhidi ya mwanamke na mtoto wa kike kama sheria ya umiliki wa aridhi na haki za mirathi.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Daniel Kimaro, ambaye alisema kuwa Katiba mpya isimuangalie mwanamke pekee kwani hata wanaume pia wananyanyasika kijinsia.

No comments:
Post a Comment