Kwa ufupi
“Sijanunuliwa, sijawaogopa watesi wangu, wala
sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata hao wanaoeneza taarifa kuwa
nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa kuninunua. Bali kimya changu
kimetokana na kufuata masharti ya daktari wangu,” ameeleza Dk Ulimboka
kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana na kununuliwa.
Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania,Steven Ulimboka
Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania,Steven Ulimboka
JESHI la Polisi nchini limeibuka na kusema linamsubiri
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka kufika
polisi na kutoa taarifa yake rasmi kuhusu tukio lililomtokea Juni 26,
mwaka huu.
Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa jeshi
hilo, Advera Senso alisema kuwa, wanamsubiri Dk Ulimboka afike polisi na
kutoa taarifa yake rasmi pamoja na ushirikiano ili wapate kujua nini
kilichotokea.
“Wakati ule hatukumhoji kwa kuwa alikuwa anaumwa
tokea hapo, hatujapata taarifa yake hivyo, sisi tunamsubiri aje kutoa
taarifa yake na atupe ushirikiano katika suala hilo,” alisema Senso na
kuongeza:
“Tunataka kujua hali yake, lakini sisi tunamsubiri aje ili tupate ushirikiano wake.”
Kabla ya polisi kutoa taarifa hiyo jana, Oktoba 28, mwaka huu, Dk Ulimboka aliibuka na kusema yuko imara na anajiaanda kuanika waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Dk Ulimboka alisema kuwa kamwe hajanunuliwa na
kuwa kwake kimya kwa muda mrefu kumetokana na kufuatilia kwa karibu
masharti ya matibabu yake na si vinginevyo.
“Sijanunuliwa, sijawaogopa watesi wangu, wala
sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata hao wanaoeneza taarifa kuwa
nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa kuninunua. Bali kimya changu
kimetokana na kufuata masharti ya daktari wangu,” ameeleza Dk Ulimboka
kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana na kununuliwa.
Dk Ulimboka alikiri kuwa amewahi kusikia taarifa
za yeye kununuliwa na kwamba huwa anajisikia vibaya anapoona kuna kundi
la watu linahaha kutaka kupotosha ukweli na kuchafua jina lake.
“Huo ni uzushi mtupu. Hata walionitesa wanajua
kuwa hawawezi kuninyamazisha au kuninunua. Wanajua sina bei katika
kutetea masilahi ya Umma. Ndiyo maana wakaamua kutumia njia ile ya
kinyama kutaka kunitoa roho yangu. Siwaogopi wanaodhuru mwili bali yule
awezaye kutoa roho. Nakuhakikishia, muda si mrefu nitaanika kila kitu
juu ya kutekwa kwangu, kuteswa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande,”
ameeleza.
Juni 26, 2012, Dk Ulimboka alitekwa kuteswa
kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa
kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.
Mwenyekiti huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania ,
aliokolewa asubuhi yake na wasamaria wema karibu na msitu huo, Bunju nje
kidogo ya Dar es Salaam.
Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Dk Ulimboka,
ambaye bado hajahojiwa na polisi wa Tanzania juu ya aliowataja,
amesisitiza kuwa alipokamatwa alikuwa na akili timamu na kwamba
waliopanga mkakati wa kumteka anawafahamu.
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI
No comments:
Post a Comment