Waakilishi wa serikali ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na wapiganaji wa M23 wanakusanyika mjini Kampala, Uganda, kwa mazungumzo.
Juma lilopita wapiganaji hao waliondoka kwenye mji wa Goma, lakini walitishia kuuteka tena iwapo madai yao hayatatimizwa.
Rais Joseph Kabila amesema atasikiliza malalamiko yao.
Watu zaidi ya nusu milioni wamekimbia makwao
katika ghasia tangu wapiganaji hao walipoasi na kutoka katika jeshi la
Congo mwezi wa Aprili.
Waziri wa taifa wa Uganda anayehusika na
mashauri ya nchi za nje, Henry Okello Oryem, amesema kuwa mazungumzo
hayo yanaweza kuendelea kwa miezi kadha kabla ya kufikia suluhu na
maafikiano kutekelezwa.
No comments:
Post a Comment