Friday, December 14, 2012

Wafufua maiti na kuitembeza mitaani

NewsImages/6711370.jpg Mmoja ya maiti ikipambwa kabla ya kufanyiwa sherehe
Wakazi wa Jimbo la Twaraj Indonesia, wamejiweka utamaduni wa kuwafufua maiti(wafu) na kuwapamba kwa kuwavisha mavazi mapya, kuwachana nywele na kuwatembeza mitaani kabla ya kuwazika tena
Dunia imejaa vituko na matukio ya ajabu, hilo limedhihirika hivi karibuni huko nchini Indonesia, katika jimbo la Twaraj, wakazi wa eneo hilo wanatamaduni ya ajabu na ngeni duniani, wakazi hao wanawafufuwa maiti kaburini na kuwavalisha nguo mapya za thamani, kuwachana nywele na kuwapamba kamalive walivyokua hai.

Wakazi hao wanakusanyika na kumfanyia sherehe kubwa maiti kabla ya kuanza msafara wa kumtebeza katika mitaa na kumrejesha kaburini alipokuwa amezikwa, wakazi hao wanamini kwamba watu waliyokufa wanahaki ya kuendelea kuishi na kujumuika nao.

katika kufanikisha zoezi hilo la kihistoria ambalo wanaimani kwa lazima kufanya ili kuonesha hishima kwa maiti na kulinda mapenzi ya kweli kwa mtu aliyekufa, kabla ya kumzika maiti anavishwa kitambaa maalum ili kuzuia mwili wa marehemu kuoza.

Mnyika: Vyombo vya uamuzi viwe huru

na Farida Ramadhani

MBUNGE wa Ubungo, John Mnyika (CHADEMA), ametaka Katiba ijayo ivipe mamlaka kamili vyombo vya uamuzi kwa lengo la kuviwezesha kufanya kazi kwa uhuru pasipo kuingiliwa na mamlaka zingine.
Mnyika alitoa maoni hayo jana wakati akichangia mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya katika mkutano uliofanyika kwenye kata ya Makurumla, jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kutaka uhuru kwa baadhi ya taasisi, pia Mnyika alitaka Katiba mpya ieleze wazi kuhusu haki ya kupata elimu, kumiliki uchumi wa nchi kwa wananchi na upatikianaji wa maji ya uhakika ni haki inayoweza kudaiwa mahakamani.
Alisema Katiba ijayo iwawezeshe wananchi kuwatimua viongozi wa ngazi ya udiwani na ubunge ikiwa wataenda kinyume na matarajio ya uwepo wao madarakani.
Alivitaja vyombo ambavyo vinapaswa kuwa huru kuwa ni pamoja Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Ofisi ya Mwendesha Mashataka (DPP) na maeneo mengine ya uamuzi kama Bunge akisema kwa sasa havina uhuru wa kutosha wa kufanya kazi pasipo kuingiliwa na muhimili mwingine.
“Leo hii wabunge tukijidai kukataa bajeti ya serikali, Rais anaweza kulivunja Bunge na yeye akabakia na urais wake; hili suala lazima liangaliwe kwa umakini katika Katiba ijayo. Tusitoe nafasi ya kumfanya mtu mmoja kuwa na nguvu zilizopitiliza,” alisema Mnyika.
Alisema kwa taasisi kama TAKUKURU, DPP na zingine za Kikatiba ni lazima wanaopata fursa ya kufanya kazi waingie kwa sifa za kuomba badala ya kuteuliwa na Rais hali inayowafanya wasiwe na uwezo wa kuhoji sehemu yenye kuhisiwa kuwa na maslahi na uongozi wa juu wa nchi.
Katika kudhibiti ufisadi na kuongeza uwajibikaji, Mnyika alitaka Katiba mpya ihimize upendo na uwe msingi mkuu wa uwajibikaji kwa kila anayepata fursa ya kuwatumikia wananchi katika ngazi yoyote.
Katika utoaji wa maoni hayo Mnyika alionyesha wasiwasi wake wa kupatikana Katiba ya wananchi kwa kile alichoeleza kuwa watakaopitia maoni ya wananchi ni tume ileile iliyoteuliwa na mtu mmoja.
Alitaka tume ya sasa ya kukusanya maoni iandae ripoti ya mapendekezo na marekebisho maalumu na kuwa kuwe na tume huru itakayosimamia maoni ya wananchi yanayokusanywa.
Katika utoaji huo wa maoni, baadhi ya wananchi walitaka nafasi ya wakuu wa wilaya na mikoa kama kuna haja ya kuwepo ziwe ni za kupigiwa kura tofauti na zilivyo sasa ambapo wahusika huteuliwa.
Mapema asubuhi, tume hiyo ilikusanya maoni kwa wakazi wa Makuburi na Mabibo ambapo walipendekeza kuwa Katiba mpya izuie uwepo wa shule na hospitali za watu binafsi.
Mbele ya mjumbe wa tume hiyo, Ester Mkwizu, mwananchi mmoja Abbas Benard alisema kuwa uwepo wa shule na hospitali za watu binafsi unaongeza matabaka katika jamii na kuzidi kukandamiza watu wa hali ya chini.
Alisema kuwa viongozi na familia zao wanatibiwa kwenye hospitali binafsi na kuacha hospitali za serikali zikiwa hazina dawa, kitu ambacho kiko hata kwenye elimu.
“Shule za serikali hazina walimu na hazina vitabu, kwa hali hii mtoto wa maskini atajikomboa kweli?” alihoji Benard.
Alipendekeza mahakama kumchagua Jaji Mkuu badala ya kuteuliwa na Rais ambaye anateuwa viongozi wengi kulingana na mamlaka aliyokuwa nayo.
Naye Masoud Kaftany, alisema kuwa Katiba ya sasa iendelee kutumika, lakini baadhi ya vitu inabidi viongezwe na vingine vipunguzwe.
Kaftany alisema kuwa anapendekeza umri wa kugombea urais uwe kuanzia miaka 40 hadi 65 wakati umri wa kugombea ubunge uwe kuanzia miaka 21 hadi 55, tofauti na ilivyokuwa katika Katiba ya zamani.
Alipendekeza kutolewa kwa viti maalumu vya wabunge na kupunguzwa kwa vyama vingi, vibakie vitatu ili kuzuia matumizi makubwa ya ruzuku ya serikali katika vyama hivyo.
Naye Harieth Raphael, alipendekeza kuwe na marekebisho ya sheria kandamizi hasa dhidi ya mwanamke na mtoto wa kike kama sheria ya umiliki wa aridhi na haki za mirathi.
Hoja hiyo iliungwa mkono na Daniel Kimaro, ambaye alisema kuwa Katiba mpya isimuangalie mwanamke pekee kwani hata wanaume pia wananyanyasika kijinsia.

KUNA TOFAUTI GANI KATI YA HIZI PICHA 2 INGAWA WOTE WANAJENGA?



NI KWELI HUU NI MWISHO WA MR.BEAN?



LONDON, ENGLAND
ANAWEZA kuwa mchekeshaji maarufu zaidi duniani kwa kipindi cha miaka 20 iliyopita, lakini kwa sasa kuna kila dalili kwamba huenda siku za kuigiza za Rowan Atkinson Mr Bean zikawa zimefika mwisho baada ya kuonyesha kuchoshwa na kazi hiyo.

Mashabiki wa Mr. Bean wanaweza kuanza kumtafuta mtu mwingine wa kuwachekesha baada ya mwigizaji huyo kutoa ishara kuwa anastaafu katika kazi hiyo iliyompatia umaarufu mkubwa na utajiri wa kutosha.
Kazi hii imekuwa ya mafanikio makubwa ya kibiashara kwangu, hata hivyo kimsingi imekuwa ngumu na inazidi kuwa ya kitoto. Hata hivyo najisikia kuendelea kuifanya kidogo zaidi, alisema akiliambia gazeti la Daily Telegraph.

Achilia mbali ukweli kwamba uwezo wa nguvu unapungua, lakini nadhani pia inahuzunisha wakati mtu unapokuwa na miaka 50 halafu inabidi uonekane kama mtoto.
Mr. Bean, ambaye sasa ana umri wa miaka 57 anasema anajisikia kuendelea kucheza filamu ambazo zitamfanya aonekane kuwa mtu makini zaidi huku akikiri kwamba filamu za ujinga alizocheza huenda zikaathiri watazamaji ambao wanamuona zaidi kama mchekeshaji kuliko mtu makini.

Jina la Mr. Bean lilipata umaarufu zaidi ya jina lake la Atkinson wakati akisoma masomo yake ya Shahada ya Uzamili (Masters) katika Chuo Kikuu cha Oxford. Kuanzia hapo aliachia tamthiliya zake zilizompatia umaarufu duniani kote kuanzia mwaka 1990-1995.

Mr. Bean alionekana kuwa na kipaji kikubwa cha kuonekana kama mtoto katika umbo la mtu mzima huku akimudu kwa ustadi mkubwa vipingamizi mbalimbali ambavyo vilimkabili katika maisha yake ya kila siku.

Mara zote alifanya kila kitu kwa umakini mkubwa bila ya kuongea neno lolote na kuwafanya watazamaji wacheke zaidi huku yeye mwenyewe akiwa kimya kama ilivyokuwa kwa mchezeshaji maarufu wa zamani, Charlie Chaplin.

Blair, Wenger wafananishwa naye
Kutokana kwa umaarufu wa tabia zake za kitoto na kijinga, watu wengi maarufu wamekuwa wakifananishwa naye pindi wanapochemka katika masuala mbalimbali yanayowahusu.
Jina Mr. Bean huchukuliwa sawa na tusi kwa wale wote wanaoonekana kichekesho mbele ya jamii.

Katuni maarufu ya Homer Simpson iliwahi kumkejeli Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza, Tony Blair ikimlinganisha na Mr. Bean kutokana na kile kilichoonekana kuburuzwa na utawala wa Marekani uliokuwa chini ya Rais wa zamani wa nchi hiyo, George Bush.

Waziri Mkuu wa zamani wa Hispania, Jose Luis Rodriguez Zapatero aliwahi kuandamwa na raia wa nchi yake waliokuwa wanamfananisha na Mr. Bean kutokana na namna alivyoonekana kuendesha mambo ovyo ovyo katika serikali yake.

Kocha maarufu wa Arsenal, Arsene Wenger, ambaye kwa sura anafanana kiasi na Mr. Bean, pia amekuwa akifananishwa na msanii huyo na baadhi ya mashabiki wa klabu hiyo kutokana na kuonekana kuishiwa mbinu za kuiendesha timu iliyoshindwa kutwaa taji lolote kwa kipindi cha miaka saba sasa.

Ana utajiri wa kutisha
Mpaka sasa, Mr. Bean ndiye staa wa televisheni mwenye utajiri mkubwa zaidi Uingereza, shukrani kwa umaarufu wake alioupata kwa uchekeshaji huo ingawa pia amekuwa akicheza filamu nyingine.

Mr. Bean ana majumba ya kifahari katika miji ya Chelsea na Oxford, huku pia akiwa anaendesha magari ya kifahari hasa yale ya mwendo wa kasi.

Anamiliki magari aina ya Honda NSX, Audi A8, Honda Civic Hybrid, Renault 5 GT Turbo, McLaren F1 na mengineyo.
Kwa ujumla anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 100 milioni (Sh 252.5 bilioni). Mpinzani wake wa karibu anatajwa kuwa mwandaaji wa vipindi vya Who Wants To Be A Millionaire, Chris Tarrant, ambaye anatajwa kuwa na utajiri unaofikia Pauni 50 milioni (Sh126.2 bilioni).

Filamu alizocheza kama Mr. Bean pekee zimempatia kiasi cha Pauni 11 milioni (Sh 27.7 bilioni) huku zikiwa zimeuzwa katika nchi 94 duniani kote. Kiasi kingine cha pesa amejikusanyia katika matangazo mbalimbali ya biashara na kampuni kubwa.

Familia yake
Mr. Bean ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne, wote wa kiume. Alizaliwa huko Consett, County Durham, England Januari 6, 1955 na baba yake ni Eric Atkinson ambaye ni mkulima. Mama yake ni Ella May. Kaka zake ni Paul (marehemu), Rodney na Rupert.
Ana mke aitwaye Sunetra Sastry aliyekuwa anafanya kazi BBC na walioana Februari 5, 1990 katika Jiji la New York, Marekani.

Wana watoto wawili na wanaishi Apethorpe, Northamptonshire ambapo pia ni karibu na uwanja wa zamani wa Arsenal, Highbury jijini London.
Kabla ya ndoa yake, Mr. Bean aliwawahi kuwa na uhusiano wa karibu na mwigizaji maarufu wa filamu, Leslie Ash.

‘Tunamsubiri Dk Ulimboka atoe taarifa’

Kwa ufupi
“Sijanunuliwa, sijawaogopa watesi wangu, wala sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata hao wanaoeneza taarifa kuwa nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa kuninunua. Bali kimya changu kimetokana na kufuata masharti ya daktari wangu,” ameeleza Dk Ulimboka kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana na kununuliwa.
Mwenyekiti wa Madaktari Tanzania,Steven Ulimboka 
JESHI la Polisi nchini limeibuka na kusema linamsubiri Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Steven Ulimboka kufika polisi na kutoa taarifa yake rasmi kuhusu tukio lililomtokea Juni 26, mwaka huu.
Akizungumza na Mwananchi jana, msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema kuwa, wanamsubiri Dk Ulimboka afike polisi na kutoa taarifa yake rasmi pamoja na ushirikiano ili wapate kujua nini kilichotokea.
“Wakati ule hatukumhoji kwa kuwa alikuwa anaumwa tokea hapo, hatujapata taarifa yake hivyo, sisi tunamsubiri aje kutoa taarifa yake na atupe ushirikiano katika suala hilo,” alisema Senso na kuongeza:
“Tunataka kujua hali yake, lakini sisi tunamsubiri aje ili tupate ushirikiano wake.”
Kabla ya polisi kutoa taarifa hiyo jana, Oktoba 28, mwaka huu, Dk Ulimboka aliibuka na kusema yuko imara na anajiaanda kuanika waliomteka, kumtesa na kisha kumtupa katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Dk Ulimboka alisema kuwa kamwe hajanunuliwa na kuwa kwake kimya kwa muda mrefu kumetokana na kufuatilia kwa karibu masharti ya matibabu yake na si vinginevyo.
“Sijanunuliwa, sijawaogopa watesi wangu, wala sijanyamazishwa kwa lolote lile. Hata hao wanaoeneza taarifa kuwa nimenunuliwa, wanajua kuwa hawana ubavu wa kuninunua. Bali kimya changu kimetokana na kufuata masharti ya daktari wangu,” ameeleza Dk Ulimboka kujibu swali iwapo kimya chake kimetokana na kununuliwa.
Dk Ulimboka alikiri kuwa amewahi kusikia taarifa za yeye kununuliwa na kwamba huwa anajisikia vibaya anapoona kuna kundi la watu linahaha kutaka kupotosha ukweli na kuchafua jina lake.  
“Huo ni uzushi mtupu. Hata walionitesa wanajua kuwa hawawezi kuninyamazisha au kuninunua. Wanajua sina bei katika kutetea masilahi ya Umma. Ndiyo maana wakaamua kutumia njia ile ya kinyama kutaka kunitoa roho yangu. Siwaogopi wanaodhuru mwili bali yule awezaye kutoa roho. Nakuhakikishia, muda si mrefu nitaanika kila kitu juu ya kutekwa kwangu, kuteswa na kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande,” ameeleza.
Juni 26, 2012, Dk Ulimboka alitekwa kuteswa kusukumizwa kwenye gari, kupigwa, kufungwa mikono na miguu, kunyofolewa kucha na kutolewa meno na hatimaye kutupwa katika msitu wa Mabwepande.
Mwenyekiti huyo wa Jumuia ya Madaktari Tanzania , aliokolewa asubuhi yake na wasamaria wema karibu na msitu huo, Bunju nje kidogo ya Dar es Salaam.
Akizungumza kwa sauti ya kujiamini, Dk Ulimboka, ambaye bado hajahojiwa na polisi wa Tanzania juu ya aliowataja, amesisitiza kuwa alipokamatwa alikuwa na akili timamu na kwamba waliopanga mkakati wa kumteka anawafahamu.
CHANZO:GAZETI LA MWANANCHI

WACHEZAJI WA ZANZIBAR WAPIGWA MARUFUKU



Timu ya soka ya Zanzibar
Timu ya soka ya Zanzibar
Shirikisho la mchezo wa Soka visiwani Zanzibar,ZFA limechukua uamuzi ambao umewashngaza sana mashabiki wengi wa soka, visiwani humo, nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti maafisa wakuu wa ZFA wamewapiga marufuku wachezaji wake wote walioshiriki katika michuano ya kuwania kombe CECAFA Senior Challenge, iliyokamilika nchini Uganda, kutoshiriki katika mechi yoyote popote duniani kwa muda usiojulikana.
Aidha ZFA limeamua kuvunja timu ya taifa maarufu kama Zanzibar Heroes, licha ya kuwa timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tatu katika michuano hiyo ya CECAFA.
Baadhi ya wachezaji hao waliopigwa marufuku ni pamoja na nyota na naodha wa Yanga, Nadir Haroub.

Kwa nini ZFA ilichukua hatua hiyo?

Nadir Haroub
Nadir Haroub naodha wa Yanga
Wachezaji hao wanakabiliwa na tuhuma za utovu wa nidhamu.
Akitoa tangazo hilo, katika makao makuu ya shirikisho hilo, makamu wa rais wa ZFA Alhaj Haji Ameir, alisema wanachama wote wa kamati kuu ya ZFA kwa kauli moja waliafikiana kuhusu hatua hiyo, ili iwe fundisho kwa wachezaji wengine.
Kamati hiyo ya ZFA iliitisha kikao cha dharura, baada ya wachezaji hao wa Zanzibar Heroes, kugawana fedha walizoshinda wakati wa michuano hiyo ya CECAFA.
Zanzibar ilimaliza katika nafasi ya tatu na hivyo kujishinda dola elfu Kumi za Kimarekani.
Ripoti zinasema fedha hizo ziligawanywa na wachezaji hao kama njia moja ya kuwasilisha malalamishi yao kwa ZFA kuhusiana na jinsi wao wanavyoshughulikiwa wakiwa kambini.
Inadaiwa kuwa wachezaji hao waliamua kugawana fedha hizo kwa madai kuwa wamekuwa wakidhulumiwa fedha zao na ZFA.
Baadhi yao wanasema ZFA huwa na mazoea ya kuchukua hela zote wanazoshinda bila hata kuwapa chochote ili hali wao ndio waliofanya kazi zaidi.

Kinyume na matarajio ya wengi kocha mkuu wa Zanzibar Heroes, Salum Bausi ambaye kujiuzulu baada ya mashindano hayo ya CECAFA, amewashangaza wengi kwa kuunga mkono, uamuzi huo akisema wachezaji hao wameharibu sifa ya Zanzibar.
Hata hivyo kuna baadhi ya wachezaji walioamua kurejesha fedha walizopewa kwa shirikisho hilo na ZFA haijatoa orodha yao.
CHANZO:BBC

HUU NDO UKWELI KUHUSU UVUMI WA MIKE TYSON KUJIBADILI JINSIA

Vyombo vya habari nchini hususan magazeti leo vimeamka na vichwa vya habari kuhusiana na taarifa iliyoenea mtandaoni kuwa bingwa wa zamani wa ndondi duniani Mike Tyson amefanyiwa upasuaji na kubadilisha jinsia yake kuwa mwanamke.
Magazeti yalioandika habari hiyo ni pamoja na Mwananchi ‘Tyson adaiwa kubadili jinsi’, gazeti la Jambo Leo ‘Tyson awa Mwanamke’ na vyombo vingine.


 Kwa kujiamini tunasema magazeti hayo yameingia ‘chaka mbaya’. Habari hiyo imeandikwa na mtandao wa http://www.newsbiscuit.com/ ambao asilimia 100 ya habari zake ni za kutunga.
Habari hiyo inasema Mike Tyson sasa ataitwa Michelle baada ya kufanyiwa upasuaji katika hospitali moja ya huko Beverley Hills nchini Marekani . Habari hii imeripotiwa na mitandao tofauti tofauti, pia gazeti la The Standard.
Habari hiyo inasema vyombo mbalimbali vya habari vimemnukuu akisema itakuwa amekamilisha ndoto yake pale atakapoanza kuona siku zake (hedhi), na kusema kuwa ili kukamilisha dhamira yake ya kuwa mwanamke’ jina lake ataitwa Michelle.
Kuna mambo mengi yanayoifanya habari hii iwe na walakini na kutufanya moja kwa moja tuamini kuwa si ya kweli. Kwa asilimia nyingi hii ni ‘hoax’ (a deliberately fabricated falsehood made to masquerade as truth.) Yaani ni habari ya ya uongo ama iliyotengenezwa ili kuifanya ionekane kama ya kweli.
Hizi ni sababu kubwa za kwanii hii ni habari ya uongo:

1. Habari hii inaonekana kutoka kwenye chanzo kimoja (newsbiscuits) na vyombo vingine vimekuwa vikiichukua kama ilivyo, neno kwa neno. Habari yenyewe ni hii:
America — Former undisputed heavyweight boxing champion of the world Mike Tyson is said to be “feeling fine” after undergoing successful gender reassignment surgery at a clinic near Beverley Hills.
Once known as “The Baddest Man on the Planet”, the boxer said having his first menstrual cycle “would be a dream come true”, and that from now on he would be known as Michelle.
“Some people might think it strange that I’m now a woman,” said Tyson, who underwent complete facial feminisation, orbital bone contouring and nasal surgery in an operation lasting over 16 hours.
‘But even at the height of my career, when pound for pound I was regarded as the best fighter in the world, I never lost touch with my feminine side and knew that one day I would grow breasts and have a vagina.’
Iron Mike was given the all-clear for gender reassignment surgery following a successful course in hormone replacement therapy which, in his autobiography, the boxer blamed for his 1996 defeat at the hands of Evander Holyfield.
Although at the time Tyson insisted he was fit enough to carry on with the fight, referee Mitch Halpern stopped the bout in the 11th round saying Tyson looked flushed, was sweating profusely and appeared to be lactating heavily from his left breast.
Tyson, said he hoped being female would finally convince the American people that his “bad-boy” days were over and he had turned over a new leaf.
2. Vyombo vinavyoheshimika kwa kuandika udaku duniani havijaandika habari hii.Kama ingekuwa kweli, hii ni habari kubwa mno kuachwa kuandikwa na mitandao kama The Sun, TMZ, mediatakeout na mingine. Hii ingekuwa habari kubwa mno pengine kuzidi hata kesi ya kulawiti watoto iliyokuwa ikimkabili Michael Jackson.
Jaribu kugoogle jina Mike Tyson kwenye sehemu ya ‘news’ na uone ni vyombo gani vimeandika habari hii. Umaarufu wa Mike Tyson duniani ungeifanya habari hii kutoandikwa na vyombo vya habari vya udaku tu bali pia mashirika makubwa kama BBC, CNN, Al-Jazeera na mengine yangetengeneza makala ndefu zenye undani mkubwa wa habari hii.
3. Akaunti zake mitandao ya kijamii hazioneshi mashabiki wake kuichukulia maanani habari hii. Tunafahamu jinsi mitandao ya kijamii inavyowaunganisha mastaa na mashabiki wao. Nenda kwenye akaunti ya Twitter ya Mike Tyson na angalia kama kuna mashabiki wanaomuuliza Tyson juu ya ukweli wa habari hii, Hakuna. Sababu ni kuwa hakuna kitu kama hicho na wengi wao hawana muda wa kuifuatilia.
4. Mike hawezi kuchukua uamuzi wa fedheha kama huo. Mike ni kitambulisho cha ujasiri na uanaume wa shoka, sio rahisi kujigeuza kuwa mwanamke, I mean come on Tyson anaweza kujigeuza kuwa mwanamke kweli?
Kwa asilimia 100 hii ni habari ya kutunga na ya uongo kama zile habari za wasanii kudaiwa kufa kwenye ajali. Bila utafiti hakuna haki ya kuongea.
Habari zingine za uongo zilizoandikwa na mtandao huo ni pamoja na ‘Abramovich amtaja Abramovich kuwa kocha wa Chelsea’, ‘Ndoa ya kwanza ya jinsia moja ya Nick Clegg na David Cameron yafungwa’, ‘Hatimaye Mungu akubali kumsaidia Malkia’, ‘Mgogoro wa mashariki ya kati wasuluhishwa kwenye Twitter’ na zingine nyingi.

CHANZO:Bongo 5

KADHI MKUU AMKANA PONDA

Kwa ufupi
Baada ya kuambiwa hivyo, Habibu alidai kuwa hakuna hata mmoja anayefamfahamu katika utendaji wa kazi za Uislamu kama kiongozi kwenye baraza lakini akawatambua kimavazi kuwa ni waumini wa Kiislamu. “Ila kwa kuona, muungwana ishalaa inamuonyesha kuwa kuna baibui, kanzu na kofia (baraghashia) inaonekana kuna Waislamu na wasio Waislamu.

  Shekhe Ponda Issa Ponda

KADHI Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Habibu (49) amekana kumfahamu Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Shekhe Ponda Issa Ponda na wafuasi wake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.

Habibu alikana kumfahamu Ponda na wafuasi wake jana Mbele ya Hakimu Mkazi, Ritha Tarimo mara baada ya kutakiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka awatazame kina Ponda na aelezee iwapo kuna mmoja aliwahi kuingia kwenye Baraza la Maulamaa wa Bakwata.

Baada ya kuambiwa hivyo, Habibu alidai kuwa hakuna hata mmoja anayefamfahamu katika utendaji wa kazi za Uislamu kama kiongozi kwenye baraza lakini akawatambua kimavazi kuwa ni waumini wa Kiislamu. “Ila kwa kuona, muungwana ishalaa inamuonyesha kuwa kuna baibui, kanzu na kofia (baraghashia) inaonekana kuna Waislamu na wasio Waislamu.”

Akiendelea kutoa ushahidi wake, Kadhi huyo aliiambia mahakama ; “Nathibitisha kuwa Kampuni ya Agritanza Ltd inamiliki lile eneo kwa Uhalali na kwamba haikupita uchochoroni ikaruka ukuta ikaingia ndani ya hilo eneo, ilifuata utaratibu na kupokea hati zote na haki yake,” alisema Habibu.

Alifafanua kuwa Baraza la Maulamaa ni chombo kinachotoa uamuzi ya mwisho na kutoa miongozo mbalimbali kwa Waislamu na kwamba Bakwata inawakilisha Waislamu wote Tanzania.

Alidai kuwa Baraza hilo la Maulamaa linaundwa na wajumbe 10 kutoka mikoa mbalimbali na kwamba mjumbe huteuliwa kutokana na kuwa na kiwango cha elimu kilichopevuka na uadilifu.

“Baraza hili linamiliki mali zinazohamishika na zisizohamishika na sisi ndiyo tunachukua uhimizwaji wa kuulizwa na kudodoswa kila kilichopo ndani ya Bakwata kwa kuwa ni lazima tuhusishwe hususan katika masuala ya elimu,” alisema Habibu.

Kwa mujibu wa maelezo ya Katiba, vikao hufanyika mara mbili kwa mwaka chini ya Mwenyekiti wa Baraza la Maulamaa pamoja na vikao vya dharura. “ Januari 3, 2011, tulifanya kikao cha kawaida ambacho kilikuwa na agenda tatu ikiwemo ya umuhimu wa kujenga chuo Kikuu cha Kiislamu ambapo wajumbe walipendekeza kijengwe katika maeneo ya Dodoma, Tanga ama Chang’ombe.”

“Kutokana na mapendekezo hayo, tuliafikiana kijengwe Chang’ombe lakini ikaonekana kuwa Chuo Kikuu cha Kiislamu kinahitaji sehemu kubwa na pale kuna Ekari 4 hapatoshi,” alisema shahidi huyo wa pili wa upande wa mashtaka.

Hivyo walimtaka Katibu Mkuu wa Baraza la Maulamaa na timu yake wafanye mchakato wa kutafuta eneo maalumu kubwa ambalo wataweza kujenga chuo hicho Kikuu cha Kiislamu na kwamba baada ya siku nne au tano walipigiwa simu na kuwa wanahitajiwa Makao Makuu (Bakwata).

Shahidi huyo alidai kuwa walipofika waliambiwa kuwa kuna kikao cha dharura na kupatiwa taarifa na Katibu Mkuu wao juu ya mchakato huo wa kutafuta eneo kuwa kampuni ya Agritanza Ltd ilijitokeza na kutaka tuwape zile ekari nne na wao watupe ekari 40 huko Kisarawe Pwani.

“Sisi tuliona ekari 40 kwa ekari 4 ni kama ardhi na mbingu na Mungu alisikia kilio chetu akawaleta hao na tukaona kabla ya mazungumzo twende tukaone, tulipofika Manshalaa eneo lilikuwa sehemu nzuri, linapendeza, linavutia na mimi nilikuwa wa kwanza kuwashawishi wenzangu tukubaliane na mabadilishano na mchakato ukafanyika,” aliongeza shahidi huyo mahakamani hapo.

Hivyo Baraza la Maulamaa liliridhia kutoa maamuzi kwa Baraza la Wadhamini kufanyika kwa mchakato na makubaliano wa maeneo hayo.
 

Wednesday, December 12, 2012

Waliopata kikombe cha Babu wazidi kupoteza maisha

Kwa ufupi
Masinde alisema idadi ya vifo vilivyotokana na Ukimwi katika wilaya hiyo katika kipindi hicho, vimeongezeka kwa asilimia mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
 IDADI ya vifo vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi katika Wilaya na Mkoa wa Geita, inasemekana imeongezeka katika kipindi cha mwaka 2011/12 kufuatia hatua ya baadhi ya wagonjwa, kuacha kutumia dawa za kupunguza makali ya virusi baada ya kwenda Loliondo kwa babu na kupata kikombe cha dawa.
Hali kadhalika kuwapo kwa shughuli za migodi ya wachimbaji wadogo na uvuvi katika Ziwa Victoria, kumechangia ongezeko la vifo vya watu kutokana na ugonjwa huo.
Imeelezwa kuwa ongezeko la shughuli za kiuchumi katika maeneo ya madini na uvuvi, ni changamoto kubwa kwa idara ya afya wilayani humo  katika kupambana na kasi ya maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Ukimwi kwa wakazi wa Geita.
Mratibu wa Mpango wa Kudhibiti Ukimwi katika Wilaya ya Geita, Patrisia Masinde, aliiambia Mwananchi jana kuwa katika kipindi cha kati ya  Januari na Novemba mwaka huu, watu 31 walipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo ambao hadi sasa haujapata tiba. Alisema watu hao ni  sehemu ya watu 131,waliokuwa wamelazwa katika vituo vya afya wakipata huduma.
Masinde alisema idadi ya vifo vilivyotokana na Ukimwi katika wilaya hiyo katika kipindi hicho, vimeongezeka kwa asilimia mbili ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Kwa mujibu wa mratibu huyo, katika kipindi hicho mwaka jana, watu waliopoteza maisha kwa ugonjwa huo walikuwa 16.
Kwa upande wake, Mratibu wa Ukimwi katika Kitengo cha Matibabu katika Wilaya ya Geita, Dk.John Mgosha alisema vifo hivyo vinatokana na baadhi ya wagonjwa waliokwenda kwa Babu wa Loliondo na kupata kikombe cha dawa, kuacha kutumia vidonge vya kuvumbaza virusi vya Ukimwi.
Alisema baadhi ya watu hao  Loliondo waliamini kwamba Mchungaji Amilikile Masapila, alikuwa na dawa ya kutibu ugonjwa wa Ukimwi licha ya kutambua kuwa hakuna dawa iliyothibitishwa na watalaamu wa afya kutibu ugonjwa huo.

MNYIKA AWATAJA MAFISADI TANESCO

Kwa ufupi
Mnyika aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa walifanya uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na kupendekeza kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza masharti kwa sababu ya mgongano wa maslahi
 MBUNGE wa Ubungo John Mnyika

MBUNGE wa Ubungo John Mnyika, ametaja majina ya watu 16 ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ambao amewahusisha na ufisadi ndani ya shirila hilo la umma.
Mnyika ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Madini na Nishati alisema watu hao ndio wanaoshirikiana kuihujumu Tanesco na kuliingiza taifa katika hasara.

Kati ya majina hayo ambayo ameyaita kuwa ni ya awamu ya kwanza wamo baadhi ya waliokuwa watendaji wa shirika hilo ambao wamesimamishwa kupisha uchunguzi unaofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG).

Alipoulizwa wiki iliyopita kuhusu uchunguzi huo, GAG Ludovick Utouh alisema uchunguzi huo umeshakamilika na kilichokuwa kikisubiriwa ni kuikabidhi ripoti hiyo kwa bodi ya Tanesco.

Mnyika aliwataja vigogo wengine watatu wa Tanesco na kueleza kuwa walifanya uzembe na kushindwa kusimamia sheria ya ununuzi wa umma na kupendekeza kampuni mbili kupewa zabuni, licha ya kuwa hazikutimiza masharti kwa sababu ya mgongano wa maslahi.

Mnyika alipendekeza vigogo hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Aliwataja watumishi wawili ambao walishindwa kutoa taarifa za ukiukaji wa vigezo vya utoaji wa zabuni namba PA/001/09/HQ/W/014 na kufanya kampuni moja kati ya hizo mblii kupewa zabuni.

Alisema watendaji hao walichangia kufanya kampuni hiyo kupewa zabuni pamoja na kwamba haikuwa na fedha na kuiwezesha kupewa malipo ya asilimia za ziada kinyume na mkataba.

Akapendekeza watendaji hao kuchuliliwa hatua za kinishamu. nMnyika aliwataja watumishi wengine sita wa Tanesco ambao kwa pamoja walifanya uamuzi uliosababisha kutolewa kwa mkataba namba PA/001/HQ/W/14 wa Machi 11,2010 kwa kampuni hiyo bila kuzingatia uwezo wa kitaalam, kifedha na hivyo kukiuka sheria ya ununuzi wa umma.

Alisema hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua ili kuwadhibiti watumishi wa umma wanaoliingiza taifa katika mikataba mibovu.

Mnyika katika taarifa yake hiyo aliwataja wafanyakazi watatu wa Tanesco akieleza kuwa walihusika katika kutoa mapendekezo yaliyowezesha kampuni ya McDonald kupewa mkataba wa zabuni kinyemela.

Mnyika alipendekeza wachukuliwe hatua za kisheria ili kuepusha Tanesco kuingia mikataba kuliongezea shirika mzigo wa gharama na kusababisha ongezeko la bei ya umeme.

Mkutano wa katiba Z’bar vurugu tupu


Kwa ufupi
Baadhi ya maeneo ambayo wanasiasa hao walivamia mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusababisha ivunjike ni Shehia za Magomeni na Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi.Hii ni mara ya kwanza ghasia kuzuka katika mikutano ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya visiwani humo.
MIKUTANO ya kukusanya maoni ya upatikanaji wa Katiba Mpya Visiwani Zanzibar, imeingia dosari baada kuzuka ghasia na baadhi ya watu kujeruhiwa kwa kuchomwa visu.
 Mwenyekiti wa tume ya mabadiliko ya katiba Jaji warioba 

Vurugu hizo ambazo chanzo chake ni siasa, zilitokana na wafuasi wa baadhi ya vyama vya siasa, kuvamia mikutano iliyokuwa ikifanyika Unguja na kusababisha hofu za kiusalama.

Baadhi ya maeneo ambayo wanasiasa hao walivamia mikutano ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusababisha ivunjike ni Shehia za Magomeni na Mpendae Mkoa wa Mjini Magharibi.Hii ni mara ya kwanza ghasia kuzuka katika mikutano ya kukusanya maoni ya Katiba Mpya visiwani humo.

Tukio la kuchomana visu, lilitokea katika Shehia ya Mpendae baada ya vurugu zilizosababishwa na vijana kuvamia mkutano uliokuwa ufanyike jana mchana.
Vijana hao walianzisha ghasia hizo baada ya kutaka kuvunja utaratibu uliokuwa umewekwa. Walitaka wakae mbele ya wengine waliokuwa wametangulia katika mkutano huo.

Hatua hiyo ilipingwa na kuibua ghasia ziliozababisha watu kadhaa kujeruhiwa kwa visu.

Tukio jingine lililovuruga mkutano huo ni lile lililotokea katika Shehia ya Magomeni, Jumatatu wiki hii baada ya kuibuka kwa mvutano baina ya makundi mawili yenye misimamo tofauti juu ya mfumo wa Muungano; kuna wanaopinga na wanaoukubali.
Misimamo hiyo imeelezwa kujikita katika misingi na sera za vyama vyao vya kisiasa.
Katika misimamo hiyo, CUF kinaamini katika Serikali ya Zanzibar na Tanganyika kila moja kuwa na mamlaka kamili na Muungano uwe wa mkataba wakati, CCM kinasimamia kwenye Serikali mbili; Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Shehia ya Magomeni
Saa mbili kabla mkutano kuanza, watu wengi walifika Uwanja wa Mzalendo ambako mkutano ulitakiwa kufanyika. Walijipanga kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na Tume ambao ni aliyewahi kufika ndiye anayetangulia kutoa maoni.

Hali hiyo ilisababisha wakazi wa Shehia hiyo waliokuwa wenyeji wa mkutano, kukosa nafasi ambayo ingewawezesha kutoa maoni kwa mazungumzo ya ana kwa ana.
Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni, Salmin Awadh Salmin, alisema hawakuwa tayari kuwa wenyeji wa mkutano ambao hawatashiriki akisema waliokuwa wamejipanga wote walifikishwa kituoni hapo kwa magari kwa lengo maalumu la kuwakosesha wenyeji kutoa maoni yao, kwa kuwa inafahamika kuwa wengi wao ni wana CCM.

Hoja hizo alizitoa kwa wajumbe wa Tume ambao pia hawakuridhishwa na hali ya usalama katika eneo hilo kutokana na vurugu zilizokuwa zikifanywa na wafuasi wa CCM na CUF.

“Kwa hali ilivyo, hatuwezi kupata utulivu utakaowezesha tufanye kazi kwa ufanisi na kumaliza mkutano kwa amani bila fujo. Natangaza rasmi kuwa leo hakuna mkutano,” Mwenyekiti wa Timu ya Tume hiyo inayokusanya maoni visiwani hapa, Profesa Mwesiga Baregu.

Akizungumza baada ya kuvunjika kwa mkutano huo, Salmin alisema waliokuwa wamefika kutoa maoni walikuwa wakitaka kunadi misimamo ya vyama vyao akisema hiyo ni hali ya kihistoria inayowakabili wakazi visiwani humo.

WHY GIVE UP?



   
 IF I knew a person who was always giving up then that’s me!
      If I was asked to mention one person that can even take her life because of giving up; I won’t think twice that would still be me.
      One day I asked myself; why should I give up all the time? Why is it that I always feel very discouraged when I do one wrong move?
       I once listened to one person preaching and he said that up there in heaven there are many souls of different people and that when your time to be born comes God calls by name and gives you a mission on Earth to fulfill- I don’t know if it’s true or not but it gave a point of thinking.
        We all have plans; thoughts and goals we want to meet; not only meet but meet them at maximum achievement. But there are times that we achieve zero or not to the level we imagined. You know it’s everybody’s right to dream, dream of anything, with any size; too small; too big they are all dreams. But can we achieve all that we dream about? Some people give up when they fail, they lose hope to try again. This is not very wise because God is the one who plans for our lives even before we plan. He knows who we are and why he created us.
         As long as sun shines at the day; the moon at night; then God is there; there is no reason to give up with God in charge for he knows our future. He won’t leave us just because we failed. He doesn’t count how many times we don’t finish the race well; what matters to him is that we took the race. If you are still alive; there is still an opportunity for you to get a second chance; still an opportunity to fix what was destroyed don’t give up.
         Why give up when you’re not alone? If you give up that means you don’t trust yourself and God who’s always by your side. He is there, he is real; and success is a must.
He never did grant anyone a peaceful and smooth journey; every champion has his own valleys different from any other. Experience shows that when your valley is more deadly the more you get promoted. Just don’t give up.
         The darker it gets the sooner the morning comes; the more the intense the pain the more the success.
Abraham-no children for years
Jacob-his only brother wanted to kill him.
Joseph- his brothers hated him.
Moses-the king wanted him dead
Jesus-killed by the Israelites (his own people)
        Everyone has his challenges; they are never the same to everyone. But what’s common is that God saves us from all those. If he raised Jesus from the dead; can’t he handle your problem!?Is it that big to him??
          Some of us just succeeded by going low first; Jesus went low as dying and got raised as high as the heavens.
         Being low does not mean you lost; it’s only a bent not the end. Struck down but not destroyed; Raise up; Gather strength; face the next level GOD was not wrong to choose you only you can play your role well
        Sometimes God breaks our spirits to savior souls. Sometimes he breaks our hearts to make us whole sometime he allows pain so as to be stronger
Sometimes he sends us failure so that we can be humble.
He sometimes takes away everything from us so as to make us learn the value of everything he gave us.
       Life is the hardest subject than all. In other subjects we learn first then test later but life is a test first; lesson later. We can’t be afraid to make mistakes; they are our only ways to learn how to be perfect.

Don’t fight your weakness; fight to win because God uses your weaknesses to raise you high.
                              Prepared by HEAVEN DAVID